Online

Friday, January 6, 2017

Mapinduzi Cup 2017: Simba SC 0-0 URA: Simba yabanwa na watoza ushuru wa Uganda

MABINGWA watetezi, URA ya Uganda wamelazimishwa sare ya 0-0 na Simba SC katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi 2017 uliopigwa uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.
Kwa sare hiyo, URA inafikisha pointi nne na italazimika kushinda mchezo wa mwisho Jumapili dhidi ya Taifa Jang’ombe ili kufuzu hatua ya nusu-fainali.
Simba SC wanafikisha pointi saba na kuzidi kujiongezea matumaini ya kucheza nusu-fainali.
Mlinda mlango Peter Manyika alianzishwa kikosi cha kwanza baada ya muda mrefu huku pia Joseph Marius Omog akiwaanzisha washambuliaji wawili Mrundi Laudit Mavugo na Juma Luizio, huku pembeni wakicheza Shizza Kichuya na Pastory Athanas lakini wakashindwa kumpa hata bao moja.
Katika mchezo mwingine wa Kundi hilo uliopigwa mapema, Jang’ombe Boys waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KVZ huku shujaa akiwa mshambuliaji wa Jang'ombe Boys Abdul-samad Kassim Ali aliyefunga hat-trick huku Salum Songoro Maulid akiifungia bao pekee la kufutia machozi KVZ.
Dondoo za mechi
Simba SC; Peter  Manyika, Janvier Bokungu, Mohammed  Hussein,  Abdi Banda, Method Mwanjali, Shiza Kichuya/Hijja Ugando dk87, Muzamil Yassin,  Juma Luizio, Laudit Mavugo/Jamal Mnyate dk80 na Pastory Athanas.
URA: Alionzi Nafian, Kulaba Jimmy,  Sekito Sam, Mumaba Allan, Ntambi Julius, Muliky Hudu/Elkanah Nkugwa dk74, Lule Jimmy, Bekota Labama, Kigongo Renald/Makogotya Robert dk54 na Kagimu Shafiq.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.