Online

Wednesday, January 11, 2017

Mapinduzi Cup 2017: Simba SC 0-0 Yanga SC (4-2 pen): Simba yaizima Yanga Mapinduzi Cup 2017, sasa kukipiga fainali na Azam FC Ijumaa

TIMU ya Simba SC imefanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi 2017, baada ya kuwatoa watani wa jadi, Yanga SC kwa mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika mchezo wa nusu-fainali uliopigwa uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.  Penalti za Simba zilifungwa na nahodha Jonas Mkude, mlinda mlango Daniel Agyei, Muzamir Yassin na mlinzi wa kimataifa wa Kongo Janvier Besala Bokungu, wakati mlinda mlango wa Yanga, Deogratius Munishi akiokoa mkwaju wa mlinzi wa Zimbabwe Method Mwanjali. Nao Yanga walipata penalti za winga Simon Msuva na kiungo wa Zimbabwe, Thabani Kamusoko wakati mlinda mlango wa imba, Daniel Agyei akiokoa penalti za Munishi na Mwinyi Hajji Mngwali.
Simba sasa itakutana na Azam FC Ijumaa katika fainali - Azam ilifuzu hatua hiyo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe katika mchezo uliotangulia.
Dondoo za mechi
Simba SC; ⁠⁠Daniel Agyei, Janvier Bokungu, MOhammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Jamal Mnyate dk72, James Kotei, Juma Luizio/Pastory Athanas dk77, Muzamir Yassin na Mohamed Ibrahim/Laudit Mavugo dk85.
Yanga SC; Deogratius Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent, Kelvin Yondan, Saidi Juma ‘Makapu’, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke/Emmanuel Martin dk63. 

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.