Online

Wednesday, January 4, 2017

Mapinduzi Cup 2017: Simba SC 1-0 KVZ: Mnyama tayari nusu-fainali, URA yaangukia pua

SIMBA SC imejikatia tiketi ya kucheza hatua ya nusu-fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KVZ katika mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar. Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na kiungo Muzamiru Yassin dakika ya 43 na kuifanya Simba SC ifikishe pointi sita baada ya kucheza mechi mbili.
Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Simba katika michuano hii inayoendelea Visiwani Zanzibar, baada ya juzi kuilaza Taifa Jang’ombe mabao 2-1.
KVZ ilimaliza pungufu mchezo huo baada ya mlinzi wake Rashid Omar Rashid kuoneshwa kadi nyekundu kufuatia kumkwatua mshambuliaji wa Simba, Pastory Athanas nje kidogo ya boksi akiwa anakwenda kufunga.
Katika mchezo wa Kundi A uliotangulia, Jang’ombe Boys iliwalaza mabingwa watetezi, URA ya Uganda mabao 2-1.
Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za Kundi B ambapo Zimamoto itakwaana na Yanga saa 10:00 Alasiri wakati Jamhuri itacheza na Azam saa 2:30 Usiku.
Dondoo muhimu za mechi
Simba SC; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohamed Hussein, Method Mwanjali, Abdi Banda, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, James Kotei, Athanas Pastory, Juma Luizio na Muzamiru Yassin.
KVZ; Abdallah Bakari, Saleh Nassor, Makarani Mluchu, Rashid Omar, Said Mohammed, Suleiman Ali, Suleiman Hassan, Suleiman Juma, Sultan Kasikasi, Mohammed Maulid na Masoud Abdllah.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.