Online

Monday, January 9, 2017

Mapinduzi Cup 2017: Simba SC 2-0 Jang'ombe Boys: D'Salaam derby yahamia Aaman, Zanzibar

WATANI wa jadi, Simba na Yanga watakutana Jumanne saa 2:15 Usiku katika uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar kwa ajili ya mchezo wa nusu-fainali ya Kombe la Mapinduzi 2017. Hiyo inafuatia baada ya Simba SC kushinda mabao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys katika mchezo wa mwisho Kundi A uliopigwa uwanja wa Amaan Visiwani humo. Matokeo hayo yanaifanya Simba imalize kileleni mwa msimamo wa kundi hilo kwa pointi 10, ikifuatiwa na Jang’ombe Boys, Taifa jang’ombe zenye pointi sita kila moja na URA yenye pointi nne.  Hivyo itakutana na Yanga iliyomaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi B nyuma ya Azam walioongoza kwa wastani wa mabao baada ya kufungana kwa pinti saba kila timu.
Katika mchezo huo nyota alikuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo aliyefunga mabao yote mawili dakika za 11 na 53.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo uliopigwa usiku Taifa Jang’ombe ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu-fainali ikiwa timu pekee kutoka Zanzibar kutinga hatua hiyo kwenye Mapinduzi Cup 2017.
Taifa imefuzu baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya URA ya Uganda huku bao pekee likifungwa na Mohamed Said. Kwa matokeo hayo Taifa Jang'ombe watakutana na Azam FC.
Dondoo za mechi
Simba SC; Peter Manyika, Janvier Besala Bokongu/Vincent Costa dk78, Mohammed Hussein,  Anbdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Hijja Ugando dk71, Muzamil Yassin/James Kotei dk46, Pastory Athanas, Laudit Mavugo/Jamal Mnayte dk55 na Juma Luizio/Moses Kitundu dk63.
Jang’ombe Boys; Hashim Ruga, Shomary Ismail, Muharami Issa, Ibrahim Said/Abubakar Ali dk72, Ali Badru, Yakoub Omar, Abdi Kassim, Khamis Makame, Hafidh Juma, Juma Ali/Ali Suleiman dk67 na Abdulsamad Ali.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.