Online

Thursday, January 5, 2017

Mapinduzi Cup 2017: Yanga SC 2-0 Zimamoto: Yanga yatinga nusu-fainali

YANGA SC imewafuata watani wao wa jadi Simba SC hatua ya nusu-fainali ya Kombe la Mapinduzi 2017 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar. Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi sita na mabao manane ya kufunga ikiwa haijaruhusu nyavu zake kuguswa na kuendelea kuongoza Kundi B. Mabao ya Yanga yakifungwa na winga Simon Happygod Msuva dakika za 11 na 21.
Katika mchezo mwingine wa Kundi A kati ya Jamhuri na Azam uliopigwa saa 2:30 usiku, ulimalizika kwa sare ya 0-0.
Mashindano hayo yataendelea leo kwa mechi mbili za Kundi A ambapo KVZ watacheza na Jang'ombe Boys saa 10:00 Alasiri vinara wa kundi hilo Simba SC watacheza na mabingwa watetezi, URA saa 2:30 usiku.
Dondoo za mechi
Yanga SC; Deogratius Munishi, Juma Abdul/Hassan Kessy dk46, Mwinyi Hajji Mngwali, Kelvin Yondani, Andrew Vincent, Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/Juma Makapu dk82, Juma Mahadhi/Oscar Joshua dk87, Haruna Niyonzima/Deus Kaseke dk62 na Emanuel Martin.
Zimamoto; Mwinyi Hamisi, Yussuf Mtuba, Hassan Ali/Nyange Othman dk83, Suleiman Juma, Shaffi Rajab/Suleiman Abbad dk32, Hajji Nahodha, Hassan Saidi, Makame Mbwana, Hakim Ali/Ally Salum dk18, Ibrahim Ahmada na Hamad Vuai/Amour Hussein dk53.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.