Online

Tuesday, January 3, 2017

Mapinduzi Cup 2017: Yanga SC 6-0 Jamhuri: Yanga hii sio ya mchezo mchezo

YANGA SC imeanza kwa kishindo michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Zanzibar baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan. Ushindi huo unaifanya Yanga iongoze Kundi B, kwa pointi tatu sawa na Azam iliyoshinda 1-0 dhidi ya Zimamoto katika mchezo wa kwanza. Winga Simon Msuva alifunga bao la kuongoza dakika ya 19 akiunganisha mpira wa kona ya nahodha Haruna Niyonzima. Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma akaifungia Yanga mabao mawili mfululizo dakika za 23 na 37.
Msuva tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao la nne dakika ya 40 akitumia makosa ya kipa.
Kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko akaifungia Yanga bao la tano dakika ya 59 akimalizia krosi ya Juma Abdul, kabla ya kiungo Juma Mahadhi⁠⁠⁠⁠⁠ aliyetokea benchi pia kipindi cha pili kuhitimisha karamu ya mabao kwa kufunga la sita dakika ya 85 kwa shuti la karibu.
Katika mchezo mwingine wa mashindano hayo uliopigwa mapema, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimamoto. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Shabani Idd dakika ya 76.
Dondoo za mechi:
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondan/Nadir Haroub dk72, Vincent Andrew, Justin Zulu, Simoni Msuva/Geoffrey Mwashiuya dk77, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Juma Mahadhi dk66, Haruna Niyonzima/Deus Kaseke dk66 na Emmanuel Martin.
Jamhuri: Omary Said, Mohammed Mgau, Mohammed Omary, Mohammed Juma, Yussuf Makame,  Greyson Gerald, Umry Bagaseka, Mbarouk  Suleiman, Mwalimu  Mohammed, Ahmed Ally na  Mussa Mbarouk.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.