Online

Monday, January 16, 2017

Serie A: Fiorentina 2-1 Juventus: Juve yavutwa Serie A

UONGOZI wa Juventus kwenye Serie A umepunguzwa hadi kufikia pointi moja baada ya mabao ya Nikola Kalinic na Milan Badelj kuipa ushindi Fiorentina wa mabao 2-1.
Foowadi wa zamani wa Blackburn Kalinic alifunga bao la kuongoza baada ya kucheza vizuri na Federico Bernardeschi.
Badelj akafunga bao la pili huku Gonzalo Higuain akifunga kwa upande wa Juventus, lakini vijana wa Paulo Sousa wakawabania zaidi.
Kwingineko kwenye Serie A, AS Roma iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Udinese, Cagliari ikaifumua Genoa mabao 4-1 huku Lazio ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Atalanta. Napoli ikaichapa Pescara mabao 3-1 huku Sampdoria ikitoka sare ya 0-0 na Empoli na Sassuolo ikashinda mabao 4-1 dhidi ya Palermo.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.