Online

Monday, January 23, 2017

Serie A: Juventus 2-0 Lazio: Juve yafanya kweli Serie A

MABINGWA wa Italia Juventus walijihakikishia utawala wao kwenye Serie A baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lazio katika mchezo uliopigwa mjini Turin.
Juve ilipata bao la kwanza ndani ya dakika tano shukrani kwa bao la Dybala. Kisha matokeo yakasoma mabao 2-0 baada ya dakika 16 baada ya mfungaji kinara Gonzalo Higuain kumalizia krosi ya Juan Cuadrado kutoka wingi ya kulia.
Kwa matokeo hayo, vijana wa Massimiliano Allegri wanaongoza ligi kwa pointi moja juu ya AS Roma, ambao waliichapa Cagliari bao 1-0, bao lililofungwa na Edin Dzeko.

Inter yakaa nafasi ya tano - Serie A round-up

Inter Milan ilipanda juu ya majirani zao AC Milan katika nafasi ya tano baada ya kuichapa timu ya pili kutoka mkiani Palermo bao 1-0 na kupata ushindi wa sita mfululizo. Bao la Inter lilifungwa na kiungo wa Ureno Joao Mario.
Kiungo wa Switzerland Blerim Dzemaili alifunga mara mbili Bologna ikiingia kwenye nusu ya pili kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Torino.
Alessandro Matri pia alifunga mara mbili Sassuolo ikishinda mabao 3-1 dhidi ya timu ya mkiani Pescara, wakati Genoa wakilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya tatu kutoka mkiani Crotone, licha ya Giovanni Simeone - mtoto wa meneja wa Atletico Madrid Diego - kufunga.
Hatari inaonekana tayari imekwama katika timu tatu za mkiani, ambapo Crotone na Palermo zina pointi 11 kutoka sehemu salama na Pescara wako nyuma zaidi kwa pointi moja.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.