Online

Monday, January 9, 2017

Serie A: Juventus 3-0 Bologna: Juventus yaweka rekodi mpya Serie A

Gonzalo Higuain alifunga mara mbili vinara Juventus wakiweka rekodi mpya ya Serie A kwa kushinda mechi 26 mfululizo katika uwanja wake wa nyumbani wakiichapa Bologna mabao 3-0 mjini Turin.
Mshambuliaji wa Argentina Higuain aliiweka mbele Juve akimalizia kazi nzuri ya Miralem Pjanic.
Paulo Dybala akafunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Bologna Marios Oikonomou kuunawa mpira.
Higuain akafunga bao la tatu kwa krosi ya Stephan Lichtsteiner na kuifanya Juve kuongoza ligi kwa pointi nne juu ya AS Roma.
Kwingineko kwenye Serie A, AS Roma walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Genoa huku bao hilo likifungwa na Armando Izzo kwa kujifunga.
Lazio ilijihakikishia nafasi yake ya nne kwenye msimamo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crotone, bao la ushindi likifungwa na Ciro Immobile.
Mlinda mlango wa England Joe Hart aliuanza mwaka 2017 kwa clean sheet baada ya Torino kulazimishwa sare ya 0-0 na Sassuolo.
Alejandro Gomez alifunga mara mbolo ndani ya dakika 23 Atalanta ikifufua matumaini ya kucheza Europa League msimu ujao baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Chievo, huku Andrea Conti na Remo Freuler wakifunga pia.
Mabao mawili ya Ivan Perisic yaliipa Inter Milan ushindi wa nne mfululizo kwenye Serie A, wakishinda mabao 2-1 dhidi ya Udinese.
AC Milan ilipata bao la dakika za lala salama lililofungwa na mshambuliaji wa Colombia Carlos Bacca wakishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Cagliari.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.