Online

Tuesday, January 17, 2017

Serie A: Torino 2-2 AC Milan: Milan yatoka nyuma na kugawana pointi

AC Milan ilipambana kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuvuna pointi moja baada ya kuilazimisha Torino sare ya mabao 2-2 kisha kupanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa Serie A.
Bao la 14 la Andrea Belotti msimu huu na bao la Marco Benassi yaliipa Torino uongozi.
Mlinda mlango kinda wa Milan Gianluigi Donnarumma, 17, alifanya kazi ya ziada kuokoa mkwaju wa penalti ya Adem Ljajic kuwazuia wenyeji kuongoza kwa mabao 3-0.
Andrea Bertolacci akapunguza idadi ya mabao kwa wageni - ambao walimaliza mchezo wakiwa 10 - kabla ya mkwaju wa penalti ya Carlos Bacca kufanya matokeo kuwa mabao 2-2.
Milan, ambayo ilimpoteza Alessio Romagnoli dakika 89 kwa kadi mbili za manjano, inakaa juu ya mahasimu wao Inter kwa pointi moja na pointi nane nyuma ya vinara Juventus.
Torino, ambayo ilitupwa nje ya Coppa Italia na wapinzani hao wiki iliyopita, wako nyuma ya vinara kwa pointi 15.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.