Online

Tuesday, January 17, 2017

Sports News: Louis van Gaa astaafu

BOSS wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal amestaafu kufundisha baada ya miaka 26.
Van Gaal, 65, hakuwa na timu ya kufundisha tangu alipofutwa kazi na United saa chache baada ya kushinda FA Cup May 2016.
"Nilidhani labda ningaliacha, kisha nikadhani itakuwa kwa muda, lakini sasa sidhani kama nitarejea kufundisha," Van Gaal alinukuliwa akizungumza na gazeti la Uholanzi De Telegraaf.
Van Gaal pia aliwahi kuzifundisha Ajax, Barcelona, Bayern Munich na AZ.
Alitoa tangazo Jumatatu baada ya kupokea tuzo ya mafanikio katika maisha kutoka kwa serikali ya Uholanzi kutokana na mchango wake kwenye soka.
Tuzo za Van Gaal
Mataji ya ligi: Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar (2008-09), Bayern Munich (2009-10)
Champions League: Ajax (1994-95)
Uefa Cup: Ajax (1991-92)
FA Cup: Manchester United (2015-16)
Alizitaja sababu za kifamilia katika maamuzi yake, ambapo De Telegraaf likisema kumechagizwa na kifo cha ghafla cha mkwewe - mume wa binti yake kilichotokea mwezi uliopita.
"Mengi yametokea katika familia yangu, unakuwa binadamu tena kutokana na mguso," aliongeza.
Pia amedai kuzipiga chini ofa kadhaa kabla kufikia uamuzi huo kutoka Mashariki ya mbali.

Safari ndefu ya mafanikio

Van Gaal alicheza nafasi ya kiungo katika klabu za Ajax, Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam na AZ baina ya 1972 na 1987 kabla ya kuhamishia akili yake kwenye ukocha, kwanza akiwa kocha msaidizi wa AZ ikafuatia nafasi hiyo katika klabu ya Ajax.
Alichukua mikoba ya Leo Beenhakker kama kocha mkuu wa Ajax mwaka 1991 na akaendelea katika kipindi cha mafanikio, akishinda taji la Ligi Kuu Uholanzi mara tatu mfululizo pamoja na Uefa Cup 1992 na Champions League 1995.
Van Gaal akahamishia mafanikio hayo katika klabu ya Barcelona ya Uhispania, akichukua mikoba ya Bobby Robson mwaka 1997 na kuiongoza timu hiyo kutwaa La Liga mara mbili mfululizo na Copa del Rey.
Nchi yake ilimuita mwaka 2000, lakini muda wake wa kwanza ulidumu chini ya miaka miwili baada ya Uholanzi kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2002, ikiwa ni mara ya kwanza kukosa fainali hizo tangu mwaka 1986.
Pia marejeo katika klabu ya Barcelona yalikuwa mafupi - miezi minane - akaondoka katikati ya msimu klabu hiyo ikiwa nafasi moja kutoka eneo la kushuka daraja.
Akaifundisha AZ Alkmaar na kuipa taji la Ligi Kuu Uholanzi msimu wa 2005-06 kabla ya kutimkia kwenye Bundesliga, ambako aliisaidia Bayern Munich kushinda taji la Bundesliga msimu wa 2009-10.
Timu ya Taifa la Uholanzi ikamhitaji tena Van Gaal mwaka 2012 na mara hii nchi hiyo ilikuwa moja kati ya timu mbili za kwanza Europe, sanjari na Italia, kufuzu fainali za Kombe la Dunia Brazil 2014, ambako walimaliza nafasi ya tatu.
Baada ya fainali hizo, alijiunga Manchester United May 2014, akisaini mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya David Moyes.
Hata hivyo, United ilimfuta kazi na nafasi yake kutwaliwa na Jose Mourinho baada ya miaka miwili kufuatia kumaliza katika nafasi ya tano kwenye Premier League msimu wa 2015-16, na taji la kwanza la FA Cup tangu 2004.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.