Online

Thursday, January 19, 2017

Sports News: Manchester United yatajwa klabu yenye pato kubwa zaidi duniani, yaimwaga Real Madrid

KLABU ya Manchester United imeibuka kinara kwa kuwa na pato kubwa kuliko klabu yoyote ya mpira wa miguu duniani msimu uliopita, kwa muijubu wa ripoti iliyochapishwa na Deloitte.
United iliipiku Real Madrid - ambayo iliongoza kwa miaka 11 - baada ya kukusanya mapato ya rekodi kwa euro 689m (paundi 515m) msimu wa 2015-16.
Klabu hiyo ya Premier League ilishuhudia mapato ya kibiashara yakiongezeka kwa euro 100m (paundi 71m).
Jumla ya mapato ya klabu zote 20 msimu wa 2015-16 yameongezeka kwa 12% hadi euro 7.4bn (paundi 6.41bn) - rekodi mpya.
Ni mara ya kwanza Manchester United kuwa kinara katika takwimu hizo za mwaka kwa mujibu wa Deloitte Football Money League tangu msimu wa 2003-04.
Real imeanguka hadi nafasi ya tatu, nyuma ya mahasimu wao wa La Liga Barcelona, ambayo inasalia katika nafasi ya pili.
Miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich ilipanda hadi nafasi ya nne na Manchester City pia ikipaa hadi nafasi ya tano - ikijikusanyia euro 524.9m (paundi 392.6m) - kutoka euro 463.5m (paundi 352.6m) msimu uliopita.
Ni mara ya kwanza kutinga tano bora.
Timu nane za Premier League zimeingia kwenye 20, zikiwa na jumla ya pato linalokaribia euro 3.2bn (paundi 2.4bn).
Mabingwa Leicester City (20) wanaingia top 20 kwa mara ya kwanza. Walivuna euro 172m (paundi 128m) - ambayo ni mara tano ya walivyoweza kukusanya misimu miwili iliyopita 2013-14.
Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham zinasalia katika nafasi za saba, nane tisa na 12, huku West Ham ikiangukia nafasi ya 18.
Orodha ya Deloitte Money League msimu wa 2015-16 - top 10
Timu (nafasi msimu uliopita)Pato kwa €m (£m kwenye mabano) 2015-16Pato 2014-15
1 (3) Manchester United689 (515.3)519.5 (395.2)
2 (2) Barcelona620.2 (463.8)560.8 (426.6)
3 (1) Real Madrid620.1 (463.8)577 (439)
4 (5) Bayern Munich592 (442.7)474 (360.6)
5 (6) Manchester City524.9 (392.6)463.5 (352.6)
6 (4) Paris St-Germain520.9 (389.6)480.8 (365.8)
7 (7) Arsenal468.5 (350.4)435.5 (331.3)
8 (8) Chelsea447.4 (334.6)420 (319.5)
9 (9) Liverpool403.8 (302)391.8 (298.1)
10 (10) Juventus341.1 (255.1)323.9 (246.4)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.