Online

Monday, January 30, 2017

Tetesi za usajili: Arsenal na Chelsea zapigania saini ya Karim Benzema, Real Madrid ipo tayari kumuuza

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Karim Benzema amepata ofa kutoka kwa klabu za Arsenal na Chelsea, kwa mujibu wa ripoti.
Diario Gol ya Uhispania imedai kuwa rais wa Real Madrid Florentino Perez yupo tayari kuachia mfaransa huyo.
Anadaiwa kushangazwa na kiwango cha Benzema, 29, ambaye hajawa na msimu mzuri kama ilivyotarajiwa. Hata hivyo ana mabao 12.
Kuondolewa kwa Real Madrid kwenye Copa del Rey hivi karibuni kunaonekana kumchukiza Perez, wakati mashabiki walipomzomea mshambuliaji huyo katika dimba la Bernabeu Jumapili kwenye mchezo dhidi ya Real Sociedad.
Perez ameripotiwa kuziambia Arsenal na Chelsea kuhusu azma yake ya kumuuza Benzema, ingawa Paris St Germain inamhitaji pia.Arsenal and Chelsea offered Karim Benzema
Benzema alizomewa wakati wa mchezo dhidi ya Real Sociedad Jumapili (Getty)
Benezema amekuwa akihusishwa kwa muda sasa kutua Emirates, lakini wakati huo huo meneja wa Chelsea Antonio Conte anatajwa kutaka kuingia sokoni kwa ajili ya mshambuliaji wa nyongeza ili kumsaidia Diego Costa.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.