Online

Sunday, January 1, 2017

Tetesi za usajili: Chelsea, Bayern Munich na Paris St-Germain zapigania saini ya Faouzi Ghoulam, Iniesta ang'ang'ania Barca, Rodriguez haondoki Bernabeu

Boss Diego Simeone hatoondoka Atletico Madrid majira ya joto kuchukua nafasi ya meneja wa Arsenal Arsene Wenger, imesema klabu hiyo. (La Sexta, via Sun)
Chelsea, Bayern Munich na Paris St-Germain zinapigana vikumbo kuinasa saini ya mlinzi wa kushoto wa Napoli Faouzi Ghoulam, 25. (Calcio Mercato)
Watford inataka kufanya uhamisho wa kiungo wa Nottingham Forest Henri Lansbury, 26. (Watford Observer)
Kiungo wa Barcelona Andres Iniesta, 32, anataka kubaki Nou Camp mpaka mwisho wa mkataba wake mwaka 2018. (Marca)
Mlinda mlango Lee Grant, 33, atahamia moja kwa moja Stoke baada ya Derby County kukubali dili lenye thamani ya paundi 1.5m pamoja na marupurupu ya paundi 750,000. (Daily Mail)
Hull City inataka kumsajili mlinzi wa kulia wa FC Groningen Hans Hateboer, 22. (Telegraaf, via Hull Daily Mail)
Kiungo wa Zenit St Petersburg Axel Witsel, 27, atachagua ama kutimkia Chinese Super League katika klabu ya Shanghai SIPG au kujiunga Juventus. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Mlinzi wa Southampton Jose Fonte, 33, analazimika "kufanya uamuzi sahihi" katika dirisha la usajili, anasema mchezaji-mwenza wa Saints na Ureno Cedric Soares, 25. Fonte anaweza kuuzwa Januari. (Southern Daily Echo)
Kiungo wa Real Madrid James Rodriguez, 25, atabaki Bernabeu, kwa mujibu wa baba yake. (AS, via Diez)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.