Online

Tuesday, January 17, 2017

Tetesi za usajili: Manchester United kukamilisha usajili mwingine wa rekodi ya dunia, mara hii kutumia paundi 100m kumsajili Antoine Griezmann, Barcelona yazungumza na wawakilishi wa Diego Costa, ipo tayari kulipa paundi 40m

KLABU ya Atletico Madrid huenda ikampoteza mshambuliaji wake nyota Antoine Griezmann majira ya joto baada ya Manchester United kuandaa kitita cha rekodi ya dunia katika usajili kwa paundi 100m, kwa mujibu wa taarifa.
Jose Mourinho anahusishwa na kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa majira ya joto na alibainisha wiki iliyopita kuwa atauza baadhi ya wachezaji mwezi Januari kwa ajili ya kupata fedha za kukamilisha uhamisho huo.
Griezmann, 25, alizungumzia kuhusu kuipenda kwake Manchester United na anaamini atakamilisha uhamisho ili kutimiza ndoto zake.
Kwa mujibu wa Independent, Atletico inaamini itamkosa mshambuliaji huyo huku ikiamini atajiunga United kwa ada ya rekodi ya dunia ambao utafikia hadi paundi 100m.PARIS, FRANCE - OCTOBER 07:  Antoine Griezmann of France reacts during warmup before the FIFA 2018 World Cup Qualifier between France and Bulgaria at Stade de France on October 7, 2016 in Paris, France .  (Photo by Aurelien Meunier/Getty Images)
Griezmann amefunga mabao 13 msimu huu (Picha: Getty)
Griezmann amefunga mabao 13 katika mechi 29 katika kikosi cha Diego Simeone msimu huu, lakini alikuwa na hasira kuzungumzia mustakabali wake.
Mshambuliaji wa zamani wa Real Sociedad alikasirika juu ya waandishi kumuuliza kuhusu uhamisho wake kutoka Vicente Calderon na kusema sasa siyo muda wake kuzungumzia maamuzi yake.
‘Msiniulize maswali haya kuhusu mustakabali wangu kwa sababu wachezaji kama Cristiano [Ronaldo], [Leo] Messi au [Gareth] Bale hakuna mtu anayewauliza kitakachotokea mwaka ujao au wapi wataenda kucheza,’ alisema Griezmann.
Wakati huo huo, miamba ya soka la Uhispania Barcelona wanataka kufanya uhamisho wa kushtukiza wa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa baada ya kutofautiana na Antonio Conte.
Costa, 28, aliwachwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichocheza na Leicester City Jumamosi, ingawa Conte anadai kuwa maamuzi hayo yalitokana na mshambuliaji huyo kusumbuliwa na mgongo.
Kichwa cha Costa sasa kimeelekea kwenye ofa kadhaa kutoka Uchina, lakini kurejea Uhispania kutakuwa kipaumbele chake.LONDON, ENGLAND - JANUARY 04: A dejected looking Diego Costa of Chelsea during the Premier League match between Tottenham Hotspur and Chelsea at White Hart Lane on January 4, 2017 in London, England. (Photo by Catherine Ivill - AMA/Getty Images)
Costa aliwachwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichocheza na Leicester (Picha: Getty)
Atletico inaweza kumkosa mshambuliaji wake Antonie Griezmann majira ya joto na wanaweza kuitumia nafasi hiyo kumshamwishi Costa arejee.
Hata hivyo, kwa mujibu wa the Independent, Barcelona ipo tayari kufanya uhamisho wa kushtukiza kwa mshambuliaji huyo na imekuwa ikimtaja kuwa mshambuliaji anayefaa sana.
Licha ya Barcelona kuwa na safu tishio ya ushambuliaji Europe, kuna hisia kwamba wanaweza kumtegemea mmoja na kuwaathiri.PAMPLONA, SPAIN - DECEMBER 10:  Luis Suarez of FC Barcelona celebrates after scoring the opening goal during the La Liga match between CA Osasuna and FC Barcelona at Sadar stadium on December 10, 2016 in Pamplona, Spain.  (Photo by David Ramos/Getty Images)
Suarez anatimiza miaka 30 mwezi huu (Picha: Getty)
Luis Suarez atatimiza miaka 30 wiki ijayo na waandamizi wa Barcelona wako tayari kubadilisha safu ya ushambuliaji.
Chelsea, kwa upande wao, wanataka kubaki na Costa kwa angalau sehemu ya msimu iliyobaki lakini wanaweza kumuuza majira ya joto.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.