Online

Thursday, January 19, 2017

Tetesi za usajili: Manchester United yakubali kumuuza Memphis Depay kwa Lyon, Everton yamkunjia Gerard Deulofeu kutua AC Milan kwa mkopo

Manchester United imekubali dili la kumuuza winga wake Memphis Depay kwa klabu ya Lyon ya Ufaransa kwa ada inayodhaniwa kwa paundi 16m ambayo itapanda hadi kufikia paundi 21.7m, kutokana na nyongeza ikiwemo Lyon kufuzu Champions League na Depay kupata mkataba mpya.
Fowadi wa Uholanzi Depay, 22, amefunga mabao saba katika mechi 53 tangu alipojiunga United kwa paundi 31m akitokea PSV Eindhoven May 2015.
Lyon inakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligue 1, pointi 11 nyuma ya vinara Monaco na pointi nane nyuma ya PSG katika nafasi ya tatu, eneo la mwisho kufuzu Champions League.
Msimu huu Depay amecheza mara nane pekee kwenye kikosi cha United, lakini amecheza dakika nane pekee tangu mwisho wa Oktoba.
Everton imepiga chini ombi la miamba ya soka la Italia AC Milan kumchukua kwa mkopo winga Gerard Deulofeu.
Deulofeu, 22, amecheza mara 13 katika kikosi cha Toffees tangu Ronald Koeman kuchukua mikoba ya umeneja Goodison Park.
Everton inasubiri kuona kama Milan itarejea na ofa mpya.
Ajax ni klabu nyingine inayomhitaji mchezaji huyo ambaye anaweza kuondoka lakini kwa mkopo.
Middlesbrough pia imekuwa ikihusishwa katika usajili wa Januari kuitaka saini ya Deulofeu.
Mhispania huyo alitua Everton kwa mkopo akitokea Barcelona kwa msimu wa 2013-14, na kuhamia moja kwa moja mwaka 2015 kwa paundi 4.3m.
Everton ingali katika hitajio la kumsajili winga wa Manchester United Memphis Depay wakati wa majira ya joto, ingawa anaweza kujiunga Lyon.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.