Online

Thursday, January 5, 2017

Tetesi za usajili: Sanchez kuondoka Arsenal, Defoe kurejea London, Diarra kufanywa chambo kumnasa Payet

WCHEZAJI wa Arsenal wana wasiwasi kuwa fowadi Alexis Sanchez, 28, yupo tayari kuondoka klabuni hapo baada ya dalili kuonesha wakati wa mchezo dhidi ya Bournemouth. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe, 34, anaweza "kurejea jijini London", anasema mchezaji-mwenza Jermaine Jenas baada ya ofa ya paundi 6m kutoka West Ham kukataliwa. (BBC Radio 5 live In Short)
Kiungo wa zamani wa Arsenal na Chelsea Lassana Diarra, 31, anaweza kutumika kama chambo kwa Marseille kumnasa kiungo wa West Ham mfaransa Dimitri Payet. (L'Equipe in French)
Mshambuliaji wa Leicester City Leonardo Ulloa, 30, hatoruhusiwa kuondoka klabuni hapo Januari. West Brom na Hull wanamuwinda. (The Sun)
Meneja wa zamani wa AC Milan, Real Madrid na England Fabio Capello anasema boss wa Manchester City Pep Guardiola anaweza kurejea Barcelona kuwa rais wa klabu. (Marca)
Stoke ipo tayari kumpa ofa ya mkataba mpya mshambuliaji Peter Crouch, 35. (Daily Telegraph)
Boss wa Southampton Claude Puel anaandaa ofa ya paundi 17m kwa fowadi wa Napoli Manolo Gabbiadini, 25. (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Juventus Simone Zaza, 25, hakutaka kujiunga West Ham kwa mkopo, anasema wakala wake. (Daily Star)
Chelsea inajiandaa kumruhusu Ruben Loftus‑Cheek, 20, kuondoka kwa mkopo mwezi huu na Brighton imeonesha nia ya kumhitaji kiungo huyo. (London Evening Standard)
Brentford imekataa ofa ya paundi 10m kutoka West Ham kwa ajili ya mshambuliaji Scott Hogan, 24. (Daily Mirror)
Aston Villa imetoa ofa ya majaribio kwa mchezaji wa Luxembourg Enes Mahmutovic, 19, kwa mujibu wa klabu ya mchezaji huyo Fola Esch. (Birmingham Mail)
Mshambuliaji wa Hearts Juanma Delgado, 27, anatarajia kufanya vipimo nchini Japan mwishoni mwa wiki hii kuelekea uhamisho wake kutua V-Varen Nagasaki. (Edinburgh Evening News)
Sevilla inakaribia kukamilisha usajili wa fowadi wa zamani wa Manchester City anayekipiga Inter Milan Stevan Jovetic, 27. (As.com in Spanish)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.