Online

Monday, January 30, 2017

Usajili: Dimitri Payet arejea Marseille kwa paundi 25m, West Ham yamjia juu

West Ham imemshutumu Dimitri Payet kwa kuonesha "nidhamu ndogo" baada ya winga huyo wa Ufaransa kurejea Marseille kwa paundi 25m.
The Hammers imesisitiza kuwa haikuwa tayari kumuuza Payet na mwenyekiti David Sullivan alisema alitaka mchezaji huyo kusalia ili kuwa "mfano" wake.
Lakini Sullivan iliongeza kuwa meneja Slaven Bilic aliamua kumuuza.
Payet amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kuicheza Ligue 1.
Kiungo mshambuliaji huyo alijiunga West Ham akitokea Marseille kwa paundi 10.7m June 2015 na kusaini mkataba mpya wa miaka mitano-na-nusu Februari 2016.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.