Online

Friday, January 6, 2017

Usajili: John Mikel Obi aitema rasmi Chelsea atimkia Uchina, Leicester City yaamilisha usajili wa kiungo wa Genk Wilfred Ndidi, Everton yatoa paundi 11m kwa Ademola Lookman

KIUNGO John Mikel Obi amevunja 'ndoa' na klabu ya Chelsea na kujiunga Chinese Super League katika klabu ya Tianjin TEDA.
Obi, 29, aliichezea Chelsea mechi 372 tangu alipojiunga mwaka 2006 lakini hakuwahi kucheza msimu huu.
Alisema ilikuwa "heshima" kucheza Stamford Bridge lakini umefika muda wa "kutafuta changamoto mpya".
Mikel alishinda mataji mawili ya Premier League, FA Cup mara nne na Champions League mara moja wakati wa utumishi wake Stamford Bridge.
"Sikupewa nafasi msimu huu kama nilivyotarajia na ningali na miaka mingi mbele ya kucheza," Mikel aliandika kwenye Twitter ikiwa ni ujmbe kwa mashabiki wa Chelsea.
Mikel anakuwa mchezaji wa pili wa Chelsea kutimkia Chinese Super League katika wiki za karibuni akitanguliwa na Oscar aliyetimkia Shanghai SIPG.
Mabingwa watetezi wa Premier League Leicester City wamefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mkabaji Wilfred Ndidi kwa ada inayotajwa kuwa paundi 15m kutoka klabu ya Genk ya Ubelgiji.
Ndidi, 20, raia wa Nigeria amekamilisha usajili wake Alhamisi na kibali cha kazi kimethibitishwa, akisaini mkataba wa miaka mitano-na-nusu.
Ndidi tayari amefanya mazoezi na klabu hiyo na anaweza kuichezea klabu hiyo Jumamosi kwenye mchezo wa FA Cup dhidi ya Everton
Ndidi aliisaidia Genk kumaliza kinara wa kwenye kundi lao kwenye Europa League na kutinga hatua ya mtoano msimu huu.
Everton imekamilisha usajili wa paundi 11m kuinasa saini ya fowadi kinda wa Charlton Athletic Ademola Lookman.
Lookman, 19,anajiunga Everton kwa mkataba wa miaka minne-na-nusu mpaka June 2021.
Mchezaji huyo wa England Under-20, ambaye alifunga mabao saba katika mechi 25 msimu huu, anakuwa usajili ghali zaidi kutoka League One.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.