Online

Wednesday, January 11, 2017

Usajili: Manchester United yamuuza Morgan Schneiderlin kwenda Everton, Arsenal yamsajili fundi magari Cohen Bramall, Holger Badstuber atua Schalke kwa mkopo

KLABU ya Manchester United imekubali kumuuza kiungo Morgan Schneiderlin kwa Everton kwa paundi 22m.
Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Schneiderlin, 27, alisajiliwa na United na aliyekuwa meneja wa wakati huo Louis van Gaal kwa paundi 25m akitokea Southampton July 2015 na akacheza mara 47 wakati huo lakini amecheza mara nane pekee chini ya Jose Mourinho msimu huu, ikiwemo michezo mitatu ya Premier League.
Everton, wakati huo huo, imekubali kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Oumar Niasse, 26, kwenda Hull.
Mshambuliaji huyo wa Senegal alisajiliwa kwa paundi 13.5m kutoka Lokomotiv Moscow Februari 2016 lakini alicheza mara saba pekee kwenye kikosi cha Toffees.
Kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull Jumanne, Mourinho alisema: "Mwenyekiti mtendaji Ed Woodward aliniambia kuwa mambo yamekamilika. Morgan anakwenda Everton.
Arsenal imethibitisha kumsajili mlinzi wa kushoto Cohen Bramall kutoka klabu ya Hednesford Town ambayo haishiriki ligi yoyote.
Bramall alifanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Gunners wiki iliyopita na sasa atakipiga katika kikosi cha klabu hiyo ya Premier League chini ya miaka 23.
Bramall, 20, alichezea Hednesford ikiwa ni kama kujifurahisha wakati akifanya kazi kwenye kiwanda cha magari ya Bentley kabla ya kukumbwa na ridanda mwezi uliopita na kuonwa na Arsenal.
Schalke imemsajili mchezaji anayewindwa na Manchester City Holger Badstuber kwa mkopo wa miezi sita kutoka Bayern Munich.
Badstuber, 27, anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati alikuwa na tatizo la majeraha na amecheza mara 18 kati ya mechi 135 za Bundesliga ndani ya miaka minne.
Boss wa City Pep Guardiola, meneja wake alipokuwa Bayern, aliwahi kuthibitisha kuvutiwa naye.
Mkataba wa Badstuber, ambaye ameutumia muda mwingi wa soka lake akiwa Bayern, unachina mwishoni mwa msimu huu.
Klabu ya Real Madrid imemtoa kwa mkopo wa miezi 18 kiungo mshambuliaji kinda wa Norway Martin Odegaard kwenda katika klabu ya Heerenveen ya Uholanzi.
Odegaard alijiunga Real kwa usajili mkubwa akiwa na umri wa miaka 16 kutoka klabu ya Stromsgodset miaka miwili iliyopita, baada ya kuwindwa na klabu kubwa barani Europe, zikiwemo Manchester United na Liverpool.
Lakini amecheza mara mbili pekee kwenye kikosi cha kwanza cha Real, akifunga mabao matano katika mechi 62 za Ligi Daraja la Tatu akiwa na kikosi B.
Ameichezea Norway ya wakubwa akiwa na umri wa miaka 15, na amecheza mara tisa hadi sasa.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.