Online

Friday, February 3, 2017

Afcon 2017: Cameroon 2-0 Ghana: Ni Cameroon v Misri fainali Afcon 2017

Cameroon itacheza na Misri kwenye fainali ya Africa Cup of Nations 2017 baada ya mabao mawili ya kipindi cha pili kuididimiza Ghana na kuihakikishia kucheza hatua hiyo.
Timu zote zilishambuliana kwa zamu huku zikipoteza nafasi kadhaa kabla ya Michael Ngadeu-Ngadjui kuyatumia makosa ya safu ya ulinzi wa Black Stars kufunga bao la kwanza dakika ya 72.
Zikisalia sekunde kadhaa mchezo huo kumalizika Christian Bassogog akafunga bao la pili kufuatia counter-attack.
Kiungo wa Panathinaikos Wakaso alimjaribu mlinda mlango wa Cameroon Fabrice Ondoa kwa free-kick, huku winga tereza wa Newcastle Atsu akipiga shuti lililopaa juu ya lango la Cameroon inchi kadhaa.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.