Online

Monday, February 6, 2017

Afcon 2017: Cameroon 2-1 Misri: Vincent Aboubakar awarejesha Cameroon kwenye soka la Afrika

Cameroon ilitoka nyuma na kuichapa Misri mabao 2-1 na kutwaa taji la tano la Africa Cup of Nations.
Mchezaji wa akiba Vincent Aboubakar alifunga bao la ushindi zikisalia dakika mbili kufikia mwisho wa mchezo huo, akipiga mpira uliompita mlinzi wa Misri Ali Gabr na kujaa wavuni.
Nicolas Nkoulou aliisawazishia Cameroon, akifunga kwa kichwa baada ya Mohamed Elneny kuifungia Misri dakika ya 22.
Bao la ushindi lililofungwa na Aboubakar liliitangaza wazi sasa Cameroon kurejea kwenye utawala wa soka la Afrika, baada ya miaka 15.
Pia inaifanya nchi hiyo kuwa nafasi ya pili katika nchi zilizofanikiwa zaidi kwenye historia ya mashindano hayo - nyuma ya Misri - na ikiwa mara ya kwanza kuwachapa Pharoahs kwenye fainali tatu za mashindano hayo.
ORODHA YA WASHINDI AFCON 2017
Mchezaji Bora wa Mashindano: Christian BASSOGOG (Cameroon)
Mchezaji Bora wa Fainali: Benjamin MOUKANDJO (Cameroon)
Tuzo ya Uungwana (Fair Play): Misri
Mfungaji Bora: Junior KABANANGA (DRC) Mabao 3
Kikosi cha Mashindano cha CAF
Mlinda mlango: Fabrice ONDOA (Cameroon)
Walinzi: Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Misri), Michael NGADEU (Cameroon)
Viungo: Charles KABORE (Burkina Faso), Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU (Ghana), Mohamed SALAH (Misri)
Washambuliaji: Christian BASSOGOG (Cameroon), Junior KABANANGA (DRC)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.