Online

Thursday, February 2, 2017

Afcon 2017: Misri 1-1 Burkina Faso (4-3 pen): Essam El Hadary shujaa Misri ikitangulia fainali Afcon 2017

MISRI imetinga fainali ya Africa Cup of Nations, baada ya kuichapa Burkina Faso kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1.
Mlinda mlango mkongwe Essam El Hadary aliihakikishia Misri ushujaa, baada ya kuokoa mkwaju wa penalti ya Bertrand Traore.
Katika muda wa kawaida Mohamed Salah alianza kuifungia Misri bao la kuongoza kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Burkina Faso.
Burkina Faso ikasawazisha kupitia kwa Aristide Bance ambaye alimalizia krosi ya Charles Kabore ambapo kufanya kwao hivyo, wanakuwa timu ya kwanza kufunga dhidi ya Misri katika fainali za mwaka huu.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.