Online

Sunday, February 26, 2017

Bundesliga: Bayern Munich 8-0 Hamburg: Robert Lewandowski apiga hat-trick Bayern ikijichimbia kileleni Bundesliga

BOSS wa Bayern Munich Carlo Ancelotti alifurahia mechi yake ya 1,000 akiwa meneja kwa ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Hamburg, ikiwa ni pamoja na hat-trick ya Robert Lewandowski.
Bayern ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 mpaka mapumziko, yaliyofungwa na Arturo Vidal na Lewandowski.
Mshambuliaji huyo wa Poland akafunga tena baada ya mapumziko, huku David Alaba akifunga bao la tano na Kingsley Coman akafunga mara mbili kabla ya Arjen Robben kufunga bao la nane.
Bayern inaongoza ligi kwa pointi tano ikifuatiwa na RB Leipzig, katika nafasi ya pili baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cologne.

Leipzig yajiimarisha - Bundesliga round-up

Leipzig, washindi wa pili wa Ligi Daraja la Pili msimu uliopita, ilijikuta ikipoteza usukani baada ya kupoteza mechi nne kati ya tisa za Bundesliga, lakini walijidhatiti wakapata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cologne.
Borussia Dortmund nayo ikashinda mabao 3-0 dhidi ya Freiburg huku klabu ya mkiani Darmstadt ikichapwa mabao 2-1 na Augsburg.
Mainz ikashinda mabao 2-0 dhidi ya Bayer Leverkusen, huku Hertha Berlin ikipaa hadi nafasi ya tano baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.