Online

Sunday, February 19, 2017

Bundesliga: Hertha Berlin 1-1 Bayern Munich: Robert Lewandowski ainusuru Bayern, Dortmund yashinda 3-0

Robert Lewandowski alifunga bao la kusawazisha dakika ya sita katika dakika sita za nyongeza vinara wa Bundesliga Bayern Munich wakiepuka kichapo kutoka kwa Hertha Berlin.
Vijana wa Carlo Ancelotti, pointi nane kileleni mwa msimamo baada ya sare, wamefungwa mara moja pekee msimu huu.
Lakini walijikuta nyuma dakika ya 21 baada ya Vedad Ibisevic kuunganisha mpira wa free-kick uliopigwa na Per Skjelbred.
Lewandowski, mfungaji bora wa Bayern, aliingia kutoka benchi na kusawazisha bao hilo dakika ya 90+6. 
Kwingineko kwenye Bundesliga, Eintracht Frankfurt, ilipata kichapo cha kwanza nyumbani msimu huu kutoka kwa timu inayotaka kujinasua kutoka mkiani ya Ingolstadt kwa mabao 2-0.
Romain Bregerie alifunga bao la kuongoza kwa wageni kwenye mchezo wa penalti mbili na kadi mbili nyekundu.
Eintracht, ambayo ilimkosa David Abraham aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Dario Lezcano kabla ya mapumziko, ilishuhudia mkwaju wa penalti ya Makoto Hasebe ukiokolewa. Pascal Gross akafanya matokeo kuwa mabao 2-0 kwa Ingolstadt, ambayo baadaye ilimkosa Mathew Leckie.
Borussia Dortmund ilipaa hadi nafasi ya tatu juu ya Eintracht kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wolfsburg.
Klabu ya mkiani Darmstadt inasalia bila ushindi wa ugenini msimu huu baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Hoffenheim, ambao mshambuliaji wa zamani wa Leicester Andrej Kramaric alifunga mara mbili.
Werder Bremen iliongeza nafasi yao ya kujinasua mkiani kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mainz. Wanasalia nafasi ya tatu kutoka mkiani, lakini pointi moja nyuma ya Hamburg, ambao Aaron Hunt alikosa mkwaju wa penalti dakika ya 88 kwenye sare ya mabao 2-2 nyumbani dhidi ya Freiburg.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.