Online

Thursday, February 2, 2017

Copa del Rey: Atletico Madrid 1-2 Barcelona: Barca yatanguliza mguu mmoja fainali Copa del Rey

Barcelona iliichapa Atletico Madrid kwenye mchezo wa kwanza wa nusu-fainali ya Copa del Rey uliopigwa kwenye dimba la Vicente Calderon.
Luis Suarez aliwaweka mbele mabingwa watetezi akikimbia na mpira kuanzia katikati ya uwanja kabla ya kuujaza kimiani.
Lionel Messi akafunga bao la pili kwa shuti kali la nje ya box.
Lakini Antoine Griezmann akawapa Atletico matumaini ya kusonga mbele kama watashinda mchezo wa marudiano Jumanne ijayo kwenye dimba la Nou Camp akifunga kwa kichwa dakika ya 59.
Alaves dhidi ya Celta Vigo ni nusu-fainali nyingine ambayo mchezo wa kwanza utapigwa Alhamisi.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.