Online

Sunday, February 26, 2017

EPL: Chelsea 3-1 Swansea City: The Blues yajikita kileleni kwa pointi 11

Chelsea iliongeza pengo katika uongozi wa Premier League hadi kufikia pointi 11 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City kwenye mchezo uliopigwa Stamford Bridge.
Cesc Fabregas alicheza mchezo wake wa 300 wa Premier League akiiweka mbele Blues, akiupitiasha mpira katikati ya miguu ya Jack Cork na kuujaza wavuni.
Wenyeji walijikuta pabaya baada ya Swansea kusawazisha kwa jaribio lao la kwanza kabla ya mapumziko - Fernando Llorente akiunganisha kwa kichwa free-kick ya Gylfi Sigurdsson.
Fabregas akagonga mwamba kabla ya Pedro kufunga bao la pili na Diego Costa akifunga bao la tatu.
Swansea walinyimwa penalti baada ya Cesar Azpilicueta kuushika mpira kwenye eneo la 18 wakati timu hizo zikiwa 1-1.
Kwingineko kwenye Premier League, Crystal Palace iliibuka na ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Middlesbrough wakati Everton ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Sunderland huku Hull City ikitoka sare ya bao 1-1 na Burnley na West Brom wakishinda mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth huku Watford wakilazimishwa sare ya bao 1-1 na West Ham.

Assist nyingine kwa Sigurdsson - dondoo

  • Hakuna mchezaji mwenye assist nyingi kwenye Premier League msimu huu zaidi ya Gylfi Sigurdsson (tisa, sawa na Kevin de Bruyne).
  • Chelsea iliruhusu bao mfululizo kwenye mechi za ligi ilizocheza nyumbani kwa mara ya kwanza chini ya Antonio Conte.
  • Swansea imeruhusu mabao 26 kwenye mechi 10 za Premier League ilizocheza ugenini, wastani wa mabao 2.6 kwa mchezo.
  • Pedro amehusika moja kwa moja katika mabao 10 katika mechi zake tisa kwa Chelsea kwenye mashindano yote (mabao saba, assist tatu).
  • Fernando Llorente amefunga mabao tisa kwenye mashindano yote msimu huu kwa Swansea, mabao matatu kwa kichwa, mabao matatu kwa mguu wa kushoto na matatu kwa mguu wa kulia.

Kifuatacho?

Chelsea ina siku tisa za kujiandaa kwa mchezo wao unaokuja ugenini dhidi ya West Ham United Jumatatu, 6 Machi. Swansea watakuwa na Burnley Jumamosi, 4 Machi.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.