Online

Friday, February 24, 2017

EPL News: Claudio Ranieri atupiwa virago Leicester City

MENEJA Claudio Ranieri amefutwa kwazi na Leicester City, miezi tisa baada ya kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji la Premier League.
The Foxes iko pointi moja juu ya mstari wa kushuka daraja huku zikisalia mechi 13.
"Bodi inataka kubadilisha uongozi, wakati ikijawa na maumivu, ni muhimu kwa matakwa ya klabu," inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Ranieri, 65, aliiongoza Foxes kutwaa taji licha ya kutopewa matumaini ya kufanya hivyo katika msimu uliopita.
Kutimuliwa kwake kunakuja chini ya saa 24 baada ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Sevilla kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League hatua ya 16.
The Foxes ilitwaa taji la Premier League kwa pointi 10 zaidi lakini imeshinda mara tano pekee msimu huu, na inaweza kuwa bingwa mtetezi wa kwanza kushuka daraja tangu mwaka 1938.
Wamepoteza mechi tano zilizopita kwenye ligi na ni timu pekee katika ligi nne za England ambayo haijafunga bao kwenye ligi mwaka 2017.
Misimu miwili iliyopita ya Leicester baada ya mechi 25
MsimuNafasiPointiUshindiKupotezaMabao ya kufungaMabao ya kufungwa
2015-161st531524727
2016-1717th215142443
"Hadhi yake ya kuwa meneja wa Leicester City aliyefanikiwa haina ubishi," iliongeza taarifa ya Foxes.
"Hata hivyo, matokeo ya ndani katika msimu wa sasa yameiweka hatarini hadhi ya klabu kwenye Premier League."
Mapema mwezi huu, Leicester walimpa heshima Muitaliano huyo, ambaaye alitajwa kuwa meneja July 2015 na kusaini mkata wa miaka mitano Agosti 2016.
"Baada ya yote ambayo Claudio Ranieri ameyafanya kwa Leicester City, kumtimua sasa hivi haikuwa busara, haisameheki na huzuni kubwa," alisema mshambuliaji wa zamani wa Foxes Gary Lineker.

Kifuatacho?

Mchezo ujao wa Leicester kwenye kupigania kusalia kwenye Premier League utakuwa dhidi ya Liverpool Jumatatu.
Meneja msaidizi Craig Shakespeare na kocha wa timu ya kwanza Mike Stowell watachukua majukumu ya kikosi hicho mpaka pale atakapopatikana meneja mpya.
Washiriki wa Ranieri Paolo Benetti na Andrea Azzalin, ambao walikuwa muhimu kwenye benchi la ufundi, wameondoka pia klabuni hapo.
"Bodi sasa itaanza mchakato na haitotoa tamko lolote mpaka mchakato huo ukamilike," iliongeza Leicester.

Mwaka mmoja (na siku tisa) katika maisha ya Ranieri

14 Februari 2016: Leicester ilichapwa mabao 2-1 ugenini na Arsenal, kichapo chao cha mwisho msimu wa 2015-16 kabla ya kucheza mechi 12 bila kupoteza.
2 May 2016: The Foxes ilitangzwa mabingwa wa England fkwa mara ya kwanza kwenye historia yao baada ya Tottenham kutoka sare na Chelsea.
16 July 2016: Kiungo N'Golo Kante anaondoka na kusaini miaka mitano kuichezea Chelsea.
13 Agosti 2016: Leicester inapoteza mchezo wao wa kwanza msimu wa 2016-17 - mabao 2-1 ugenini kwa Hull City.
15 Oktoba 2016: The Foxes yachapwa mabao 3-0 na vinara Chelsea Stamford Bridge.
22 Novemba 2016: Leicester wanajihakikishia uongozi kwenye kundi lao la Champions League wakisaliwa na mchezo mmoja.
18 Disemba 2016: Ranieri anatajwa Kocha Bora wa Mwaka na BBC Sports Personality.
7 Februari 2017: Baada ya kushinda mechi mbili katika mechi 15 za ligi, Leicester yampa Ranieri sapoti yao.
22 Februari 2017: The Foxes inachapwa mabao 2-1 na Sevilla kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League hatua ya 16.
23 Februari 2017: Ranieri anatimuliwa.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.