Online

Thursday, February 2, 2017

EPL: West Ham United 0-4 Manchester City: Gabriel Jesus aweka rekodi Premier League, United yabanwa OT

Gabriel Jesus alifunga bao lake la kwanza akiwa na Manchester City the Citizen wakiwachapa West Ham mabao 4-0 kwenye mchezo wa Premier League uliopigwa London Stadium.
City, ambao waliwaacha mshambuliaji Sergio Aguero na mlinda mlango Claudio Bravo kwenye benchi, walitangulia kufunga baada ya Kevin de Bruyne kucheza pasi za kugongeana na Jesus.
Dakika nne baadaye, wakaongeza bao baada ya Leroy Sane kuwaramba chenga walinzi wawili na krosi yake  ikaunganishwa na David Silva.
Na mchezo ulikuwa mzuri zaidi kwa City kabla ya mapumziko ambapo Raheem Sterling alimalizia mpira wa Jesus kufunga bao la tatu.
Yaya Toure akaongeza bao la nne baada ya mapumziko kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Hammers Jose Fonte kumuangusha Sterling.
Kwingineko kwenye Premier League, Manchester United ilishindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani Old Trafford baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Hull City huku Stoke City ikibanwa pia katika dimba la Britannia baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Everton.

Dondoo za mechi - Toure aweka rekodi nzuri

  • Gabriel Jesus anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga na kutoa assist kwenye mechi ya kwanza kuanza kwenye Premier League katika kikosi cha Manchester City.
  • Jesus pia anakuwa mchezaji wa pili kinda kutoka Brazil kufunga bao lake la kwanza kwenye Premier League (miaka 19 na siku 304), nyuma ya Rafael aliyeifungia Manchester United Novemba 2008 (miaka 18 na siku 122).
  • David Silva alifunga bao lake la tatu la Premier League ugenini dhidi ya West Ham - jumla kubwa ya mabao ya ugenini dhidi ya mpinzani mwingine kwenye mashindano hayo.
  • West Ham imefungwa mabao manne au zaidi kwenye mechi tatu kati ya 12 za Premier League ilizocheza London Stadium - namba sawa na mchezo wa mwisho wa 106 kwenye uwanja wa Upton Park.
  • Yaya Toure amefunga penalti zake zote 11 za Premier League - rekodi ya 100% kwenye mashindano hayo.
  • Katika mchezo wake wa 50 kwenye Premier League, Kevin de Bruyne alirekodi uhusika wa bao lake la 30 kwenye mashindano (mabao 11, assist 19).
  • City imefunga mabao tisa kwenye mechi mbili katika mashindano yote ilizocheza London Stadium - nusu ya mabao ambayo West Ham imefunga (18) katika mechi 17.

Kifuatacho?

Klabu zote zinarejea kwenye Premier League mwishoni mwa wiki.
City watawaalika Swansea Jumapili, wakati Hammers wataifuata Southampton Jumamosi.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.