Online

Wednesday, February 22, 2017

Europa League: 3 viwanjani leo Europa League: Match Preview: Saint-Etienne v Manchester United: United kuwakosa Rooney, Phil Jones na Herrera

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amewachwa kwenye kikosi cha Manchester United kitakachocheza mchezo wa marudiano ya Europa League hatua ya 32 Jumatano ugenini dhidi ya Saint-Etienne.
Rooney, 31, ameikosa michezo minne ya United kutokana na majeraha ya mguu na hajasafiri na timu hiyo licha ya kufanya mazoezi Jumanne.
Timothy Fosu-Mensah amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 20 lakini walinzi wa pembeni Luke Shaw na Matteo Darmian wamekosekana.
Vijana wa Jose Mourinho wana faida ya mabao 3-0 waliyoyapata kutoka kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford.
Kiungo Ander Herrera amefungiwa na mlinzi Phil Jones atakosekana kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Kufuatia safari ya Ufaransa, United itapambana na Southampton Jumapili kwenye fainali ya EFL Cup itakayopigwa uwanja wa Wembley.
Kocha wa Saint-Etienne Christophe Galtier anaamini timu yake ingali bado kwenye nafasi ya kusonga mbele licha ya hat-trick ya Zlatan Ibrahimovic kwenye mchezo wa kwanza.
Alisema: "Tuna kazi nzito lakini siyo pingu. Tutacheza kwenye hali ya hewa nyingine kubwa. Uwanja utajaa.
"Tunaiheshimu hadhira yetu. Haiwezekani kwetu kutocheza vizuri katika matumaini yaliyopo ya kufuzu. Kwenye mchezo lolote linaweza kutokea."
Michezo mingine ya Europa League Jumatano ni Schalke itakuwa nyumbani dhidi ya PAOK Salonika wakati Fenerbah├že wataialika FK Krasnodar.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.