Online

Friday, February 17, 2017

Europa League: Manchester United 3-0 Saint-Etienne: Zlatan Ibrahimovic apiga zote tatu

Zlatan Ibrahimovic alifunga hat-trick Manchester United ikishinda mchezo wa kwanza wa Europa League hatua ya 32 dhidi ya Saint-Etienne ya Ufaransa.
Ibrahimovic alifunga bao la kwanza kwa free-kick iliyomchanganya mlinda mlango Stephane Ruffier na akafunga bao la pili baada ya kazi nzuri kutoka Marcus Rashford, akakamilisha hat-trick kwa mkwaju wa penalti.
Saint-Etienne ilikaribia kuisababishia matatizo United hasa baada ya mapumziko, hasa kupitia kwa Romain Hamouma, wakati Henri Saivet na Nolan Roux both wakipiga mashuti yasiyokuwa na uelekeo.
Ruffier aliokoa mara mbili mashuti ya Juan Mata na Anthony Martial, wakati Paul Pogba akipiga kichwa kilichogonga mwamba.
Timu hizo zitakutana kwenye mchezo wa marudiano Jumatano, 22 Februari.

Kifuatacho?

Manchester United itasafiri kuifuata Blackburn Rovers kwenye mchezo wa FA Cup Jumapili, wakati Saint-Etienne itapambana na Montpellier kwenye Ligue 1 siku hiyo.

United yarejea zama zake - dondoo

  • Zlatan Ibrahimovic amehusika na mabao 18 kwenye mechi 17 kwenye dimba la Old Trafford msimu huu (mabao 12, assist sita).
  • Jose Mourinho ameweka clean sheet tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2011 alipokuwa bosi wa Real Madrid.
  • Mlinda mlango Sergio Romero ameweka clean sheet sita mfululizo kwa United na hajafungwa bao tangu mkwaju wa penalti ya Alex Revell kwa Northampton Septemba 2016.
  • The Red Devils imeshinda mechi tatu mfululizo za Europe bila kuruhusu bao kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2010 chini ya Sir Alex Ferguson.
  • Licha ya kutokuwa na shuti lililolenga lango mpaka dakika ya 30, Saint-Etienne walikuwa na mashuti 11 kipindi cha kwanza, mengi zaidi kwa wapinzani katika dimba la Old Trafford kipindi cha kwanza tangu Athletic Bilbao ilipokuwa na mashuti 13 Machi 2013.
Matokeo yote ya Europa League

MwenyejiMabaoMgeni
FC Krasnodar1-0Fenerbahce
Ludogorets Razgrad1-2FC Copenhagen
Olympiacos0-0Osmanlispor FK
FC Rostov4-0Sparta Prague
AZ Alkmaar1-4Lyon
Astra Giurgiu2-2Genk
Borussia M.Gladbach0-1Fiorentina
Celta Vigo0-1Shakhtar Donetsk
Gent1-0Tottenham
Villarreal0-4Roma
Anderlecht2-0Zenit St. Petersburg
PAOK Thessaloniki FC0-3Schalke 04
Manchester United3-0Saint-Etienne
Hapoel Beer Sheva1-3Besiktas
Athletic Club3-2APOEL Nicosia
Legia Warszawa0-0Ajax

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.