Online

Sunday, February 19, 2017

FA Cup: Blackburn Rovers v Manchester United: United hatihati kuwakosa Henrikh Mkhitaryan, Wayne Rooney na Michael Carrick

Blackburn itaingia dimbani bila Hope Akpan na Elliott Bennett, ambao wamefungiwa, wakati Lucas Joao haruhusiwi kucheza.
Fowadi anayekipiga klabuni hapo kwa mkopo Sam Gallagher pia atakosekana baada ya kuhitaji wiki 12 kutibu jeraha la goti wakati Tommy Hoban na Corry Evans hawako fiti.
Henrikh Mkhitaryan (mgonjwa), Wayne Rooney na Michael Carrick (wanasumbuliwa na misuli) huenda wakakosekana baada ya kuukosa mchezo wa Manchester United kwenye Europa League.
Lakini mlinzi Phil Jones huenda akawa fiti baada ya majeraha ya mguu.

Mchezo mwingine kwenye FA Cup utakuwa Fulham dhidi ya Tottenham utakaopigwa kwenye dimba la Craven Cottage.

Blackburn Rovers v Manchester United

Uso-kwa-uso
 • Mara ya mwisho timu hizi kukutana kwenye FA Cup ilikuwa msimu wa 1984-85 ambapo Manchester United ilishinda mabao 2-0 raundi ya tano - walikwenda mbele zaidi na kushinda kombe hilo msimu huo.
 • Ushindi wa mwisho kwa Blackburn kwenye FA Cup dhidi ya Manchester United ulikuwa mabao 2-0 nyumbani msimu wa 1927-28 raundi ya sita. Rovers walishinda kombe hilo mwaka huo.
 • United haijafungwa kwenye mechi sita zilizopita kutembelea Blackburn (W3, D3).
Blackburn Rovers
 • Blackburn imeshinda mara moja katika mechi nne zilizopita (D1, L2).
 • Rovers imepoteza mara moja kwenye mechi zao tano za mwisho kwenye dimba la Ewood Park kwenye mashindano yote (W3 D1).
 • Wameshinda FA Cup mara sita.
 • Wes Brown alicheza fainali tatu za FA Cup akiwa na Manchester United, alishinda kombe hilo mwaka 2004 lakini akamaliza kwa kichapo miaka ya 2005 na 2007.
Manchester United
 • Manchester United imeshinda mara nne kati ya tano kwenye mashindano yote.
 • Wamepoteza mara moja kwenye mechi tisa za ugenini zilizopita kwenye mashindano yote (W6, D2).
 • United imeshinda mechi zote za FA Cup msimu huu kwa mabao 4-0 (dhidi ya timu za Championship Reading na Wigan).
 • Hawajapoteza mchezo wa FA Cup ugenini dhidi ya timu za madaraja ya chini tangu kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Harry Redknapp wa timu ya daraja la tatu Bournemouth raundi ya tatu msimu wa 1983-84.
 • Anthony Martial amehusika katika mabao tisa kwenye mechi zake nane za FA Cup (mabao matatu, assist sita).

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.