Online

Monday, February 20, 2017

FA Cup: Chelsea kuialika Manchester United Darajani robo-fainali FA Cup

VINARA wa Premier League Chelsea watawaalika mabingwa watetezi Manchester United kwenye mchezo wa robo-fainali ya FA Cup.
Na timu ambayo haishiriki ligi yoyote Lincoln City, ambayo iliiondosha kwenye mashindano Burnley kwenye dimba la Turf Moor, itawafuata Arsenal kama the Gunners wataichapa Sutton United Jumatatu usiku.
Kwingineko, Manchester City watacheza na Middlesbrough kama watafanikiwa kuichapa Huddersfield Town kwenye mchezo wa marudiano baada ya sare ya 0-0 Jumamosi.
Na timu ya League One Millwall watakuwa na safari fupi kaskazini mwa London kuwafuata Tottenham kwenye raundi ijayo ya mashindano hayo, ambayo itachezwa baina ya Machi 10-13.

FA Cup: hatua ya robo-fainali

Chelsea v Manchester United
Middlesbrough v Huddersfield/Manchester City
Tottenham v Millwall
Sutton United/Arsenal v Lincoln CityFA Cup quarter-final draw: Chelsea host Man Utd as Lincoln discover incredible tie
Man United itaifuata Chelsea (Picha: Getty)
Lincoln wana uhakika wa kucheza tobo-fainali ama na miamba ya Premier League au timu-mwenza isiyokuwa katika Sutton.
Safari kuifuata Arsenal itakuwa kubwa zaidi kwenye historia yao wakati dhidi ya Sutton inaweza kuipa nafasi ya kutinga nusu-fainali ya FA Cup.Lincoln City fans celebrate as they watch the Emirates FA Cup, Quarter Final draw in the Travis Perkins bar at Sincil Bank, Lincoln. PRESS ASSOCIATION Photo. Picture date: Sunday February 19, 2017. See PA story SOCCER Lincoln. Photo credit should read: Richard Sellers/PA Wire
Mashabiki wa Lincoln wakishangilia (Picha: Richard Sellers/PA Wire)

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.