Online

Tuesday, February 7, 2017

FA Cup Tanzania: Simba SC v African Lyon Yanga SC v Kiluvya United, Ndanda FC yapelekwa Majimaji

RAUNDI ya Sita ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) 2016/17, inatarajia kuanza Februari 24, 2017 kwa michezo minne kuchezwa siku hiyo. Michezo hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza na Stand United ya Shinyanga katika uwanja wa kaitaba mjini Bukoba.
Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam FC na Mtibwa Sugar wakikutana Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.
Jumapili Februari 26, Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons ikipambana na Mbeya City zote za Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Jumatano Machi 1, 2017 Simba SC itacheza na African Lyon kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam wakati Machi 7, Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Ratiba kamili:
Madini FC v JKT Ruvu
Kagera Sugar v Stand United
The Mighty Elephant v Ndanda FC
Azam FC v Mtibwa Sugar
Mbao FC v Toto Africans
Tanzania Prisons v Mbeya City Council FC
Simba SC v African Lyon
Yanga SC v Kiluvya United 

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.