Online

Sunday, February 19, 2017

FA Cup: Wolverhampton Wanderers 0-2 Chelsea: Pedro na Costa waipeleka Chelsea robo-fainali FA Cup, Leicester yachapwa

VINARA wa Premier League Chelsea wametinga robo-fainali ya FA Cup kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers kwenye mchezo uliopigwa Molineux.
Wolves, pointi tano juu ya mstari wa hatari kwenye Championship, walikuwa wazuri kipindi cha kwanza baada ya George Saville kupiga kichwa langoni mwa Chelsea lakini kiligonga nguzo.
Safu ya ulinzi wa Chelsea ikajikuta majaribuni kabla wageni hao kukaa sawa, wakiilazimisha Wolves kurudi nyuma na kumruhusu Pedro kufunga bao la kuongoza.
Diego Costa akaifungia Chelsea bao la pili likiwa bao lake la 16 msimu huu.
Droo ya robo-fainali itafanyika Jumapili.
Kwingineko kwenye FA Cup, Burnley ilichapwa bao 1-0 na Lincoln City wakati Manchester City ikilazimishwa sare ya 0-0 na Huddersfield na Middlesbrough ikaichapa Oxford United mabao 3-2 na Millwall ikailaza Leicester City kwa bao 1-0.

Pedro aendelea kutamba FA Cup - dondoo za mechi

  • Pedro sasa amefunga kwenye raundi ya tatu, nne na tano za mashindano ya FA Cup msimu huu.
  • Mhispania huyo amefunga mabao saba kwenye mechi 10 za kimashindano.
  • Diego Costa alimaliza ukame wa mechi nne bila bao (dakika 413).
  • Chelsea sasa imeshinda mechi 10 kati ya 11 kwenye mashindano yote dhidi ya Wolves (L1), ikiwa na clean sheet nane kwenye mechi hizo.
  • Vijana wa Antonio Conte wameshindwa kufunga kwenye mchezo mmoja pekee kati ya 12 ilizocheza ugenini kwenye mashindano yote.
  • Huu ni ushindi wa 24 kwa Chelsea msimu wa 2016-17 kwenye mashindano yote, licha ya kucheza mara 31 (uwiano wa ushindi wa 77%). Walishinda 20/53 msimu wa 2015-16 (38%).
  • Hiki kinakuwa kichapo cha nne mfululizo kwa Wolves kwenye mashindano yote na hawakupata bao kwenye mechi tatu za mwisho.

Kifuatacho?

Chelsea itawaalika Swansea City Jumamosi, 25 Februari kwenye mchezo wa Premier League wakati Wolves watawaalika Birmingham City Ijumaa, 24 Februari.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.