Online

Monday, February 20, 2017

La Liga: Barcelona 2-1 Leganes: Messi aiokoa Barca

BAO la mkwaju wa penalti dakika ya 90 uliopigwa na Lionel Messi liliisaidia Barca kuichapa Leganes mabao 2-1 na kuifanya Barcelona kurejea kwenye nafasi ya pili msimamo wa La Liga.
Mabingwa watetezi walijikuta pabaya tena baada ya Jumanne iliyopita kuchapwa mabao 4-0 na Paris St-Germain kwenye Champions League na mara hii wakitakiwa kumshukuru kipa Marc-Andre ter Stegen kwa kuokoa hatari nyingi.
Messi aliifungia Barca bao la kuongoza dakika za mapema, kabla ya Unai Lopez kusawazishaa.
Fowadi wa Barcelona kisha akafunga bao la kuongoza na la ushindi dakika za lala salama.
Ushindi unawafanya Barcelona kusogea juu ya Sevilla kwa pointi mbili katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga. Wana pointi 51, moja pungufu dhidi ya vinara Real Madrid ambao wana mechi mbili mkononi.
Kwingineko kwenye La Liga, Real Sociedad walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Villarreal wakati Valencia wakishinda mabao 2-0 dhidi ya Ath Bilbao na Celta Vigo wakiirarua Osasuna mabao 3-0.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.