Online

Sunday, February 26, 2017

La Liga: Real Betis 1-2 Sevilla: Sevilla yalingana pointi na Real Madrid kileleni La Liga

SEVILLA ilipambana kutoka nyuma na kuichapa Real Betis mabao 2-1 kwenye derby na kulingana pointi na vinara wa La Liga Real Madrid.
Mlinzi wa kushoto wa Betis Riza Durmisi aliwafungia wenyeji bao la kuongoza kwa free-kick, kabla ya Gabriel Mercado kuisawazishia Sevilla baada ya mapumziko.
Vicente Iborra akafunga bao la ushindi baada ya Steven N'Zonzi kubabatizwa na free-kick ya Samir Nasri.
Real Madrid wanacheza Jumapili, sawa na Barcelona.
Vijana wa Zinedine Zidane watakuwa dhidi ya Villarreal wakati Barca, ambao sasa wapo katika nafasi ya tatu, watasafiri kuifuata Atletico Madrid.
Katika mchezo wa mapema Jumamosi, Alaves ilitoka nyuma na kuichapa Valencia mabao 2-1.
Alaves, ambayo watacheza na Barca kwenye fainali ya Copa del Rey 26 May, imesogea hadi nafasi ya 10, wakati Valencia, ambayo waliitandika Real Madrid mabao 2-1 Jumatano, wanasalia katika nafasi ya 14th.
Kwingineko kwenye La Liga, Leganes iliisukumia Deportivo La Coruna katika nafasi ya 16 kwa ushindi wa mabao 4-0, wakati timu ya nafasi ya saba Eibar iliendeleza msimu wao mzuri kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Malaga, ambao wanasalia katika nafasi ya 13.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.