Online

Sunday, February 19, 2017

La Liga: Real Madrid 2-0 Espanyol: Bale arejea kwa kishindo

GARETH Bale alifunga bao la aina yake katika kurejea uwanjani baada ya zaidi ya miezi mitatu kuwa nje ya uwanja kutokana na kuumia enka vinara wa La Liga Real Madrid wakiichapa Espanyol mabao 2-0.


Fowadi wa Wales, akiingia kipindi cha pili, aliiwahi pasi ya Isco kabla ya kukimbia na mpira katikati ya walinzi wa wageni na kumtungua mlinda mlango Diego Lopez.
Alvaro Morata alikuwa wa kwanza kuifungia Real kwa kichwa akiunganisha krosi ya Isco.
Ushindi huo unawafanya vinara Real kuwa juu ya Sevilla, ambao waliichapa Eibar 2-0, kwa pointi tatu.
Barcelona, pointi moja zaidi nyuma katika nafasi ya tatu, watawaalika Leganes Jumapili.
Zidane alifanya mabadiliko saba kutoka kwenye timu iliyoichapa Napoli mabao 3-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League hatua ya 16 Jumatano iliyopita, akiwaacha nje mlinda mlango namba moja Keylor Navas, kiungo Luka Modric na mshambuliaji Karim Benzema.

Kwingineko kwenye La Liga

Gameiro apiga hat-trick ndani ya dakika 5

Kevin Gameiro alifunga hat-trick ndani ya dakika tano timu ya nafasi ya nne Atletico Madrid ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Sporting Gijon.
Mabao ya mchezaji huyo wa akiba aliyeingia kipindi cha pili yalimhakikishia Diego Simeone ushindi katika dimba la El Molinon kwa mara ya kwanza tangu 2008.
Yannick Carrasco alifunga ndani ya sekunde 20 baada ya kipindi cha pili kuanza kuipa Atletico uongozi kabla Sergio Alvarez kusawazisha dakika mbili baadaye.
Gameiro aliingia uwanjani dakika ya 61 na kufunga bao lake la kwanza dakika ya 79 - akimalizia pasi ya Antoine Griezmann.
Mfaransa huyo aliyenunuliwa kwa paundi 28m akafunga bao la pili na kukamilisha hat-trick dakika ya 84.

Sarabia na Vitolo wairejesha Sevilla nafasi ya pili

Sevilla ilijiandaa kwa mchezo wa Jumatano wa Champions League hatua ya mtoano dhidi ya Leicester kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Eibar, kwa maboa ya Pablo Sarabia na Vitolo.
Fowadi wa zamani wa Manchester City Stevan Jovetic alitengeneza mabao yote, akipiga awali krosi iliyozaa bao lililofungwa na Sarabia dakika ya 30, na akapiga pasi kwa bao la pili lililofungwa na Vitolo.
Ushindi unawaweka Sevilla kwenye nafasi ya pili, ingawa Barcelona wanaweza kurejea juu yao wakiepuka kichapo nyumbani kutoka kwa Leganes.
Katika mchezo mwingine Deportivo La Coruña ilichapwa bao 1-0 na Alavés.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.