Online

Monday, February 27, 2017

La Liga: Villarreal 2-3 Real Madrid: Madrid yarejea kileleni La Liga

Real Madrid ilipambana kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kurekodi ushindi wa mabao 3-2 ugenini dhidi ya Villarreal, ushindi ambao uliwafanya warejee kileleni mwa msimamo wa La Liga.
Mambo yalikuwa mabao 2-1 wakati ambapo mchezaji wa Villarreal Bruno kudaiwa kuushika mpira kwenye box, ingawa halikuwa kusudio lake.
Cristiano Ronaldo akafanya matokeo kuwa mabao 2-2 kwa mkwaju wa penalti baada ya Gareth Bale kuanza kuifungia Real.
Mchezaji wa akiba Alvaro Morata akafunga bao la ushindi zikisalia dakika saba mchezo huo kumalizika.
Real ina pointi 55, pointi moja juu ya Barcelona ambao waliichapa Atletico Madrid mabao 2-1 kwenye mchezo wa mapema Jumapili. Real pia wana mchezo mmoja mkononi dhidi ya Sevilla, ambayo inakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na pointi 52.
Kwingineko kwenye La Liga, mabao mawili ya Lionel Messi yalitosha kuipa Barcelona ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Atletico Madrid, huku Espanyol wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Osasuna wakati Athletic Bilbao wakiibamiza Granada mabao 3-1 na Sporting Gijón wakilazmishwa sare ya bao 1-1 na Celta Vigo.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.