Online

Monday, February 27, 2017

League Cup: Manchester United 3-2 Southampton: Zlatan Ibrahimovic ndiyo jina la mchezo

BAO la dakika za lala salama lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic liliipa Manchester United taji la EFL Cup na mafanikio ya kwanza kwa meneja Jose Mourinho tangu alipoteuliwa kuwa meneja, wakiizidi maarifa Southampton kwenye fainali iliyopigwa Wembley.
Southampton walikuwa imara zaidi kwennye fainali hii lakini waliangushwa baada ya bao lao kukataliwa wakidaiwa kuotea - na ushujaa ukaenda kwa Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 ambaye amefikisha mabao 26 msimu huu.
Mshambuliaji wa Saints Manolo Gabbiadiani alifunga bao lililokataliwa akidaiwa kuotea kabla ya kufunga na kuwafanya United kuchukua uongozi kwa mabao mawili yaliyofungwa na Ibrahimovic dakika ya 19 na Jesse Lingard dakika saba kabla ya mapumziko.
Southampton, kiwango chao kikiwalinda, walisawazisha kupitia kwa Gabbiadini.
Oriel Romeu akafanya kazi nzuri kabla ya Ibrahimovic kufunga bao la ushindi akimalizia pasi ya Ander Herrera zikisalia dakika tatu kuipa United ushindi.

Kwa nini Lingard anapapenda Wembley - dondoo

  • Jesse Lingard amefunga katika kila mchezo kati ya michezo mitatu aliyocheza Wembley kwa Manchester United (fainali ya FA Cup 2016, Ngao ya Jamii na fainali ya League Cup msimu huu).
  • Jose Mourinho ameshinda fainali zote nne za League Cup alizocheza (2005, 2007, 2015 na 2017).
  • Zlatan Ibrahimovic sasa amefunga mabao sita kwenye fainali tano za ndani (mabao manne kwenye mechi nne akiwa na PSG).
  • Haya yalikuwa mabao ya 25 na 26 ya Ibrahimovic msimu huu kwenye mashindano yote, mecgi kuliko mchezaji yeyote wa Premier League msimu huu.
  • Bao la kwanza la Ibrahimovic lilikuwa na kwanza kwenye nyavu za Southampton kwenye League Cup msimu huu, ikicheza dakika 468 bila kuruhusu bao kwenye mashindano hayo.
  • Manolo Gabbiadini ni mchezaji wa nne kutoka Italia kufunga kwenye fainali ya League Cup (wengine ni Fabrizio Ravanelli, Roberto di Matteo naa Fabio Borini).
  • Gabbiadini ni mchezaji wa pili kufunga mara mbili kwenye fainali ya League Cup dhidi ya Manchester United baada ya Dean Saunders.
  • Manchester United imeshinda kila mchezo kati ya michezo sita iliyocheza Wembley.
  • Ni Liverpool (8) pekee imeshinda League Cup mara nyingi zaidi ya Manchester United (5).

Kifuatacho?

Shughuli itahamia Old Trafford kwa Manchester United ambapo watawakaribisha Bournemouth kwenye mchezo wa Premier League Jumamosi.
Siku hiyo hiyo, Southampton watakuwa na mchezo dhidi ya Watford utakaopigwa Vicarage Road.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.