Online

Monday, February 27, 2017

Ligue 1: Marseille 1-5 Paris St-Germain: PSG yainyemelea Monaco Ligue 1, Memphis Depay apiga mbili Lyon ikiua 5-0

Paris St-Germain iliifanyia kitu mbaya Marseille kwa kuichapa mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa Le Classique na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligue 1.
Marquinhos alifunga bao la kuongoza, huku Edinson Cavani akifunga bao la pili baada ya kumzidi ujanja kipa Yohann Pele.
Lucas Moura na mchezaji wa akiba Julian Draxler nao wakafunga, kabla ya mlinzi Rod Fanni kufunga bao la kufutia machozi kwa wenyeji.
Lakini Blaise Matuidi akaongeza bao la tano na kuifanya Marseille ikubali kichapo kikubwa cha kwanza nyumbani kwenye Ligue 1 tangu mwaka 1953.
PSG, inalisaka taji la tano mfululizo kwenye Ligue 1, ikikamata nafasi ya pili juu ya Nice kwa tofauti ya mabao na pointi tatu nyuma ya vinara Monaco.
Mapema katika Ligue 1, winga wa zamani wa Manchester United Memphis Depay alifunga mara mbili Lyon ikiichapa Metz mabao 5-0 huku Saint-√Čtienne ikilala kwa bao 1-0 kutoka kwa Caen.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.