Online

Sunday, February 26, 2017

Ligue 1: Monaco 2-1 Guingamp: Monaco yatakata Ufaransa

VINARA wa Ligue 1 Monaco walisogea kwa pointi tatu zaidi kileleni baada ya ushindi dhidi ya Guingamp.
Mlinzi wa Monaco Kamil Glik alifunga bao la kuongoza akiunganisha free-kick ya Thomas Lemar, akisaidiwa na makosa ya winga wa Guingamp Jimmy Briand kushindwa kuokoa.
Falcao akakosa bao kwa mpira wake uliokosa uelekeo kabla ya mshambuliaji kinda Kylian Mbappe, 18, kuangshwa kwenye box na Karl-Johan Johnsson.
Fabinho akafunga kwa penalti na kufanya matokeo kuwa mabao 2-0, kabla ya Etienne Didot kufunga bao la kufutia machozi.
Nice inayokamata nafasi ya pili ililingana pointi baada ya timu ya Leonardo Jardim kushinda mabao 2-1 dhidi ya Montpellier Ijumaa.
Mabingwa watetezi Paris St-Germain, katika nafasi ya tatu, sasa wako pointi sita nyuma ya Monaco lakini wanaweza kuzipunguza kama wataishinda Marseille Jumapili.
Kwingineko kwenye Ligue 1, Bordeaux ilipaa hadi nafasi ya tano kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Lille ambao waliwakosa wachezaji wawili waliotolewa nje zikisalia dakika 10.
Timu ya mkiani Lorient ilichapwa bao 1-0 na Rennes, ambao wanapaa hadi nafasi ya nane, Angers kaichapa Bastia mabao 3-0, na Nancy ikalazimishwa sare ya 0-0 na Toulouse.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.