Online

Wednesday, February 8, 2017

Serie A: AS Roma 4-0 Fiorentina: Edin Dzeko apiga mbili Roma ikiifukuzia Juventus

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester City Edin Dzeko alifunga mara mbili AS Roma ikiichapa Fiorentina mabao 4-0 na kuweka rekodi mpya ya klabu hiyo.
Klabu hiyo ya mji mkuu wa Italia imeshinda mechi 14 za nyumbani kwenye Serie A, ikivunja rekodi yake iliyoiweka tangu mwaka 1930.
Dzeko, ambaye sasa ni mfungaji kinara wa ligi hiyo akiwa na mabao 17, alitangulia kufunga kabla Federico Fazio kuongeza la pili kwa kichwa.
Radja Nainggolan akafunga bao la tatu akimalizia krosi ya Kevin Strootman na Dzeko akayatumia makosa ya Davide Astori kufunga bao la nne.
Roma, ambayo inapaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Serie A, wako nyuma ya vinara Juventus kwa pointi nne, ingawa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya mabingwa hao.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.