Online

Monday, February 6, 2017

Serie A: Juventus 1-0 Inter Milan: Juve hiyo yaendelea kuchanua kileleni mwa Serie A

BAO la Juan Cuadrado liliwasaidia vinara wa Serie A Juventus kuwachapa Inter Milan bao 1-0 na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa pointi sita.
Cuadrado alifunga bao pekee kwa shuti kali la umbali wa yadi 25 baada ya walinzi wa Inter kushindwa kuokoa mpira wa kona.
Pia Juve walikosa nafasi kadhaa kupitia kwa Paulo Dybala na Miralem Pjanic.
Inter, ambao walikuwa wameshinda mechi zao saba za Serie A, walimkosa Ivan Perisic ambaye alioneshwa kadi mbili za manjano wakati Juventus wangaliweza kufunga mabao zaidi huku shuti kali la Dybala likigonga nguzo ya goli, na free-kick ya Pjanic ikiokolewa na mlinda mlango wa Inter Samir Handanovic.
Inter walikuwa na nafasi kadhaa, ambapo Roberto Gagliardini kupiga shuti lililokosa uelekeo kisha akapiga kichwa kilichodakwa na Gianluigi Buffon.
Joao Mario pia Mauro Icardi wakapoteza nafasi kwa Nerazzurri, ambayo sasa imeshuka hadi nafasi ya tano kwenye msimamo.
Juve - mabingwa kwa misimu mitano mfululizo - wako pointi sita juu ya Napoli, wakiwa na mchezo mkononi.
Mapema Jumapili, kiungo wa Lazio Marco Parolo alifunga mara nne kwenye ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Pescara na AC Milan wakalala kwa bao 1-0 kutoka kwa Sampdoria, kichapo cha nne mfululizo. Atalanta ikaichapa Cagliari mabao 2-0 huku Chievo ikitoka sare ya 0-0 na Udinese. Nayo Empoli ikatoka sare ya bao 1-1 na Torino, wakati Genoa ikichapwa bao 1-0 na Sassuolo na Palermo ikashinda bao 1-0 dhidi ya Crotone.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.