Online

Sunday, February 26, 2017

Serie A: Juventus 2-0 Empoli: Juve haikamatiki Serie A

Juventus ilijikita kileleni mwa msimamo wa Serie A kwa pointi 10 zaidi baada ya ushindi wa 30 mfululizo nyumbani wakiitandika Empoli mabao 2-0.
Vijana wa Massimiliano Allegri, wakilisaka taji la sita mfululizo, walipata bao la kuongoza baada ya Lukasz Skorupski kujifunga kufuatia mpira wa kichwa uliopigwa na Mario Mandzukic.
Juve walipoteza nafasi kadhaa, lakini Alex Sandro akaihakikishia ushindi kwa kufunga bao la pili.
Roma wanaweza kupunguza pointi dhidi yao watakapocheza na Inter Milan Jumapili.
Mapema kwenye Serie A, Atalanta iliichapa Napoli mabao 2-0 na kukaa katika nafasi ya nne, licha ya kumkosa kiungo Frank Kessie aliyeoneshwa kadi mbili za manjano.
Mabao ya Atalanta yalifungwa na mlinzi Mattia Caldara.
Kichapo kinawafanya Napoli kukaa nafasi ya tatu, pointi 12 nyuma ya vinara Juve, na sasa wako pointi tatu juu ya Atalanta, ambao walimaliza katika nafasi ya 13 msimu uliopita.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.