Online

Friday, February 3, 2017

Sports News: Baada ya miaka 21 hatimaye Frank 'Super' Lampard atundika njumu

KIUNGO wa zamani wa Chelsea na England Frank Lampard amestaafu soka, baada ya miaka 21 uwanjani.
Lampard, 38, ambaye alicheza mwaka uliopita katika klabu ya New York City kwenye Major League Soccer nchini Marekani, alitangaza kustaafu kwenye mitandao ya kijamii Alhamisi.
Lampard alicheza mara 649 akiwa na Chelsea na mechi 106 kwenye kikosi cha England.
"Nimepokea ofa nyingi kuendelea kucheza, katika umri wa miaka 38 nahisi sasa ni wakati wa kuanza sura nyingine katika maisha yangu," alisema Lampard.
"Nina furaha na FA kwa nafasi ya kujifunza juu ya sifa za ukocha wangu na natazamia kutumia nafasi nyingi nje ya uwanja ambazo maamuzi haya itazifungua."
Lampard alishinda mataji makubwa 11, yakiwemo matatu ya Premier League na Champions League mwaka 2012. Lampard pia alishinda FA Cup mara nne, League Cup mara mbili na Europa League.

Rekodi za Lampard

  • Ni Ryan Giggs (632) na Gareth Barry (615) wamecheza mara nyingi zaidi kwenye Premier League dhidi ya Lampard (609).
  • Jumla ya mabao yake 177 kwenye Premier League yanamfanya kushika nafasi ya nne nyuma ya Alan Shearer, Wayne Rooney na Andy Cole.
  • Amefunga mabao mengi nje ya box kuliko mchezaji yeyote wa Premier League (41).
  • Lampard amefunga dhidi ya timu 39 tofauti kwenye Premier League - ni rekodi.
  • Hakuna mchezaji wa England aliyefunga penalti nyingi zaidi ya Lampard (tisa), ukiondoa hatua ya upigaji wa penalti. 
Lampard alijiunga Chelsea akitokea klabu ya utotoni West Ham kwa ada ya paundi 11m mwaka 2001.
Mabao yake 211 ya kihistoria kwa klabu yaliisaidia Blues kushinda Champions League, Premier League mara tatu, FA Cup mara nne, League Cup mara mbili, Europa League na Ngao ya Jamii.
Alikuwa mchezaji muhimu kwa Jose Mourinho wakati Chelsea inatwaa taji la kwanza la Premier League, akifunga mabao 13 ukijumlisha na mabao ya mechi ya ushindi wa taji - mabao 2-0 dhidi ya Bolton Aprili 2005.
Angaongeza mabao 16 kwenye ligi msimu uliofuata Chelsea ikitetea taji lake, akimaliza nafasi ya pili nyuma ya fowadi wa Barcelona Ronaldinho kwenye tuzo za Ballon d'Or na Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa.
Lampard alifunga mabao 10 au zaidi kwenye Premier League katika misimu 10 mfululizo akiwa na Chelsea, akifunga mabao 22 wakati Chelsea ikitwaa taji la Premier League kwa mara ya tatu msimu wa 2009-10.
Yakafuata mafanikio ya Champions League msimu wa 2011-12 Lampard akiwa nahodha wa Chelsea kwenye matuta dhidi ya Bayern Munich baada ya kukosekana kwa John Terry.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.