Online

Tuesday, February 21, 2017

UEFA: 2 viwanjani leo UEFA: Manchester City v Monaco: Vincent Kompany, Kun Aguero ndani

NAHODHA wa Manchester City Vincent Kompany hatokabiliana na Monaco kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League hatua ya mtoano Jumanne usiku.
Mlinzi huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, 30, anaendelea kupona baada ya kuumia goti kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace Novemba.
Boss wa City Pep Guardiola ataamua Jumanne ama kumuanzisha Claudio Bravo au Willy Caballero langoni.
Kiungo wa Monaco Gabriel Boschilia atakosekana kutokana na kuwa majeruhi ambayo yatamuweka nje hadi mwisho wa msimu.

Falcao wa moto

Monaco inaongoza msimamo wa Ligue 1 na ndiyo timu inayoongoza kwa kupachika mabao kuliko timu yoyote kwenye Ligi Kuu tano bora Europe, wakifunga mabao 76 kwenye mechi 28.
Mshambuliaji Radamel Falcao anarejea England akiwa na mabao 19 kwenye mechi 25 kwenye mashindano yote msimu huu.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia, 31, alifunga mabao manne kwenye mechi 29 alizoichezea Manchester United msimu wa 2014-15, na bao moja alipokuwa kwa mkopo Chelsea msimu uliofuata.
"Monaco ni timu iliyokuwa na mafanikio katika kufunga mabao Europe, hivyo hii ratiba ngumu," alisema Guardiola.
"Tunaangalia mbele kucheza dhidi yao. Ni timu nzuri."

Nafasi ya Aguero kung'ara?

Kutokana na Gabriel Jesus kusemwa atakaa nje kwa kipindi cha hadi miezi mitatu baada ya kuvunjika mfupa wa mguu, Sergio Aguero anatarajiwa kuhifadhi nafasi yake katika ushambuliaji.
Aguero, 28, alishindwa kuisaidia City kwenye sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Huddersfield kwenye FA Cup raundi ya tano Jumamosi iliyopita.
Hata hivyo, Muargentina huyo amefunga mabao 18 msimu huu, yakiwemo mabao matatu kwenye Champions League, na Guardiola amebainisha umuhimu wake kwenye timu yake.
"Sergio ana uzoefu wa kutosha," alisema.
"Tutazungumza naye kama wachezaji-wenza wote kumshawishi katika mechi hizi mbili, dakika 180, hatutokuwa na uwezo wa kucheza vizuri kwa sababu katika kwango hiki inahitajika sana kwenye Champions League.
"Haya ni moja kati ya mashindano bora kucheza na tutajitahidi."
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Bayer 04 Leverkusen dhidi ya Atletico Madrid utakaopigwa katika dimba la BayArena, Ujerumani.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.