Online

Wednesday, February 22, 2017

UEFA: Bayer 04 Leverkusen 2-4 Atletico Madrid: Atletico kumaliza kazi Vicente Calderon Jumatano, 15 Machi

ATLETICO Madrid ilifunga mabao manne ugenini na kujihakikishia kuimarisha utawala wake wa Champions League hatua ya 16 dhidi ya Bayer Leverkusen.
Saul Niguez aliwafungia wageni bao la kuongoza, kabla ya Antoine Griezmann kuongeza bao la pili akiunganisha pasi ya Kevin Gameiro kufuatia makosa ya mlinzi wa Leverkusen Omer Toprak.
Wendell akagonga mwamba wake katika harakati za kuokoa krosi ya Felipe Luis huku mlinda mlango Bernd Leno akiokoa hatari za Griezmann.
Karim Bellarabi akaifungia Leverkusen mapema kipindi cha pili, lakini mkwaju wa penalti ya Gameiro ukawapa Atletico faida ya mabao mawili kabla ya Stefan Savic kujifunga.
Mchezaji wa akiba Fernando Torres akaifungia Atletico bao la nne.
Mechi ya marudiano itapigwa uwanja wa Vicente Calderon Jumatano, 15 Machi.
Katika mechi ngingine iliyopigwa Etihad Manchester City ilishinda mabao 5-3 dhidi ya Monaco.

Havertz afuata nyayo za Draxler - dondoo

  • Antoine Griezmann amefunga mara 11 kwa Atletico Madrid tangu mwanzo wa msimu uliopita Champions League, mabao sita zaidi ya mchezaji yeyote kwa klabu hiyo.
  • Griezmann ni mfungaji kinara wa Atletico kwenye Champions League/European Cup akiwa na mabao 13, akimzidi Luis Aragones (12).
  • Atletico alifunga mabao manne kwenye mechi ya ugenini kwenye Champions League kwa mara ya kwanza tangu Septemba 1996 (4-1 dhidi ya Widzew Lodz).
  • Mchezo huu ulimaliza mbio za mechi nane za Champions League kwa Leverkusen bila kufungwa (imeshinda mbili, sare sita).
  • Mabao yote matano ya Saul Niguez kwenye Champions League yamekuwa mabao ya kwanza kwenye mechi hizo.
  • Gabi alitoa assist yake ya kwanza kwenye Champions League tangu Novemba 2015 (mbili dhidi ya Galatasaray).
  • Karim Bellarabi alifunga bao lake la kwanza la Champions League tangu Machi 2012 (kichapo cha mabao 7-1 kutoka kwa Barcelona).
  • Kai Havertz anakuwa mchezaji kinda kuanza kwa Bayer Leverkusen kwenye mchezo wa Champions League (miaka 17, siku 255) na ni kinda wa pili wa Ujerumani kufanya hivyo baada ya Julian Draxler.

Kifuatacho?

Timu zote zinarejea kwenye mechi za ligi mwishoni mwa wiki. Leverkusen itaialika Mainz kwenye Bundesliga Jumamosi, wkati Atletico watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Barcelona Jumapili.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.