Online

Wednesday, February 15, 2017

UEFA: Benfica 1-0 Borussia Dortmund: Pierre-Emerick Aubameyang akosa penalti Dortmund ikilizwa ugenini

Kostas Mitroglou aliipa Benfica faida ya bao moja kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League hatua ya 16 dhidi ya Borussia Dortmund.
Mitroglou alifunga bao pekee kwenye mchezo huo kwa mabingwa wa Ureno akiunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na Luisao.
Mshambuliaji wa Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang alipiga mkwaju wa penalti ambao ulidakwa na mlinda mlango wa Benfica Ederson baada ya Ljubomir Fejsa kuunawa mpira katika box.
Dortmund walikuwa vinara wa mabao kwenye hatua ya makundi, lakini walishindwa kupata bao.
Dortmund watakuwa wenyeji wa mchezo wa pili 8 Machi.
Kwingineko, Paris St-Germain waliichabanga Barcelona mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza hatua ya mtoano uliopigwa jijini Paris, Ufaransa.

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.