Online

Tuesday, February 14, 2017

UEFA: Benfica v Borussia Dortmund: Licha ya kuwa majeruhi Borussia Dortmund yamjumuisha Mario Gotze kwenye kikosi

MAJERUHI Mario Gotze amejumuishwa kwenye kikosi cha Borussia Dortmund ambacho kitateremka kwenye dimba la Estádio da Luz Jumanne kwa ajili ya mchezo wa awali hatua ya mtoano wa Champions League dhidi ya wenyeji Benfica.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, anasumbuliwa na majeraha ya mguu ambayo yalimuweka nje kwenye mchezo ambao Dortmund walichapwa mabao 2-1 na timu ya mkiani mwa msimamo wa Bundesliga Darmstadt.
Marcel Schmelzer na Lukasz Piszczek, ambao waliukosa mchezo dhidi ya Darmstadt kutokana na majeraha, nao watakuwepo.
Eduardo Salvio anaweza kurejea kwenye kikosi cha Benfica baada ya kupona enka.
Hata hivyo, mshambuliaji wa Brazil Jonas huenda akakosekana baada ya kukosa mazoezi ya Jumatatu.

Borussia Dortmund wana matumaini ya Europe

Kiwango cha Dortmund kimekuwa cha kusua sua tangu Disemba, ambapo walishinda mara mbili pekee kwenye mechi tisa kwenye mashindano yote.
Ilipoteza mara moja pekee kwenye kipindi hicho - kichapo cha Jumamosi kutoka kwa Darmstadt - lakini bosi wa Dortmund Thomas Tuchel ana matumaini ya kupata ushindi nchini Ureno.
"Tuko mbali sana na matarajio yetu na tunatakiwa kukiri Darmstadt walistahili ushindi," alisema.
Mchezo mwingine utapigwa kwenye dimba la Parc des Princes ambapo mabingwa wa Uhispania Barcelona watakuwa wageni wa mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain.

Benfica v Borussia Dortmund

Dondoo za mechi

  • Borussia Dortmund iliiondoa Benfica kwenye raundi ya kwanza ya European Cup msimu wa 1963-64, mchezo pekee uliopita baina yao. Walichapwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza, lakini walishinda kwa mabao 5-0 Ujerumani kwenye mchezo wa marudiano.
  • Benfica imeshinda mara moja katika mechi 15 za European Cup/Champions League zilizopita dhidi ya klabu za Ujerumani (D5 L9), ilikuwa dhidi ya Kaiserslautern Novemba 1998.
  • Borussia Dortmund imefuzu hatua ya mtoano wa Champions League katika kila mwaka kwenye misimu minne iliyopita, ikimaliza kinara kila msimu.
  • Borussia Dortmund ni moja kati ya timu sita ambazo hazijapigika kwenye msimu huu wa Champions League (W4 D2). Ilishinda mechi zote mapema msimu huu dhidi ya timu nyingine kutoka jiji la Lisbon, Sporting (mabao 2-1 Ureno, 1-0 Ugerumani).
  • Hata hivyo, Dortmund imepoteza mechi sita kati ya nane zilizopita kwenye htua ya mtoano wa Champions League (W2).

No comments :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. The Chief - All Rights Reserved.